Monday, July 5, 2010

ni kweli uzazi wa mwanamke umelaaniwa?

Mwanzo 3:7-19, utakutana na laana ya mungu kwa wanadamu lakini zaidi kwa mwanamke. Mungu alimlaani mwanamke kuwa atazaa kwa uchungu na atakuwa mtegemezi mkuubwa kwa Mumewe, hivi ni kweli mwanamke kalaaniwa?? uzazi wa mwanamke umelaaniwa? lakini je kama ni kweli unaamini uzazi huo umelaaniwa, je sisi ambao ni wazaliwa wa uzazi huo??

najiuliza eti mwanaume via Adam kalaaniwa kula jasho lake, ni kweli tulipaswa kuishi bila kutoa jasho?? maisha bila jasho yangekuwa na maana kweli??

ila sasa Hii ni kwa wale wanaoamini Mungu wa biblia pekee kwani kuna wengne wanaoamini kuwa kuzaliwa binadamu ni bahatai, baraka na ni upendeleo mkuubwa kutoka kwa mungu na kwamba mwanamke ni kiumbe wa ajabu na wa aina yake mbele za Mungu kwa uwezo wake wa kuzaa, kunyonyesha kulea nk vinavyodhirisha upendo ambako Mungu ndo upendo wenyewe

4 comments:

Anonymous said...

Hivi huyu mungu wa Biblia ni yupi? maana hata mungu mwenyewe amelaaniwa.
(wagalatia 3-13)

Ikiwa wanaadam pamoja na mungu mwenyewe (KRISTO) wote ni walaaniwa, je kwa kufuata maandiko ya biblia ni kweli tutaingia katika ufalme wa mbinguni ambao ndio uzima wa milele?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@anony, kwanza umekosea kuandika wagalatia 3-13, sijui unamaanisha nini nafikiri kuna kitu kinakosekana au hakijaandikwa vizuri,

ila swali lako ni kwa kufuata biblia, duh naomba nisikujibu kwani sijui kama nina utaalamu wa kuitafsiri biblia hii

Anonymous said...

@Kamala,
kama binadamu nakubali na ninaheshimu kukosolewa kwani hakuna mkamilifu ispokua mungu pekee. mkuu naomba unirekebishe nilipokosea.

Kiswahili ni lugha isiyojitosheleza, kwa mfano, nguo huitwa mavazi unapozivaa, unapozivua huitwa mavuzi.

mada ni laana, na huwa naogopa sana laana. ndio nikauliza mungu wa biblia ni yupi?
Andiko linasema,nanukulu:
"Kristo alitukomboa katika laana ya torati,kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti"

Kwa mujibu wa Biblia Kristo ni mungu. sasa nifanyeje ili kuepuka laana?

Bwana yesu akubariki sana.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony, nimekuelewa na sijui niseme nini kwamba ufanyeje kuepuka laana, sikubali kwamba umelaaniwa wala nini. miminakuona poa kabisaa. ukikubali hiyolaani utakuwa umejilaani mkuu au??

itafute kweli ikuweke huru, kumbuku Mungu yumo ndani mwako na jinsi ya kumfikia ni kupitia humondani, utakuwa umeiepuka laana ukilijua nakuliishi hilo