Friday, July 2, 2010

nimefanikiwa kujua kuhusu miungu ya wahaya


nasoma kitabu alichokiandika m-Misionary mmoja aliyeishi kwenye Buahaya kindom miaka ya 1940. katika kitabu hicho nimefanikiwa kujua kuhusu Miungu ya wahaya wafanyiayo tambiko na nikaona ni Bora niweke hapa na wewe uone

alikuwepo Muungu mkuu aitwaye Wamara, ilikuwa ni pamoja na kuabudu watu waliokufa, karibia familia nyingi zina wamara kwani huwa zinaenda kufanya matambiko kama vile kupalilia kaburi au kulitembelea zikiamini zitapata baraka


Mzimu wa pili ni Mungu wa Maji aitwaye Mugasha, huyu utawala maji yoote yaani mito, maziwa nk. na huyu ana tambiko zake kwa wavuvi na wakazi wa karibu na maji.


na Muungu tatu ambaye ni wa nuru au mwanga aitwaye kazooba, huyu ni muungu wa Jua, mwezi na hata nyota.
ukikutana na wahaya waitwao Kazooba, kawamara, wamara, mugasha nk ujue chanzo chao ni mizimu hiyo.

interesting ehe!! ila mimi ni mtu wa kiroho aka seeker after truth na kwa hiyo siamini katika haya na wala siyafuati hata kama ni utamaduni wangu. ila usiniige unless umekua kiroho vinginevyo utapotea.

hakuna tofauti saana kati ya mizimu hii na dini za kigeni. kwa mfano wahaya walienda kutambika milimani, kwenye miti mikuubwa (ebigabilo) na ndivyo waumini waendavyo kwenye majumba makuubwa (kanisa, hekalu) na kupiga magoti mbele ya sanamu wakiongozwa na padre, mchungaji au mwinjilisiti kama vila wahaya walivyoongozwa na Igaba, bachweezi, embandwa nk ila tambiko hizi kama zilivyo dini, vyote huamini juu ya nguvu ipitayonguvu zote ila sasa njia n ngumu watambikaji walalavyo na hirizi, ndivyo wafuasi wa dini lalavyo na biblia au vitabu vya dini.

4 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

hii bomba sana!

chib said...

Mie naiita pipe kabisa!

Anonymous said...

Kazi ipo, huu ni upotevu kama ilivyo kwa Biblia na Ukristo kwa ujumla.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony, umelonga ila sasa unajaribu kuwaambia waliogizani kuwa kuna mwanga, hawatakuamini na ukiwalazimisha watakupiga mawe