Monday, July 12, 2010

shikamoo!, amani iwe kwenu!

hivi nani aligundua au kuvumbua salamu tuzitumiazo katika jamii kama vile shikamoo? hivi tunaelewa maana ya salamu hii na chanzo chake?? hatuna salamu nyingine nzuri za kutakiana mema?

niliambiwa kuwa salamu ya shikamoo ilianzia kwa wakoroni waarabu ambao walisalimiwa na watumwa kwa kushikwa miguu na kusema 'nimeshika miguu yako (shikamoo' na yule mkoloniakajibu 'mara-haba' kwamba hata ukishika mara mia hazitoshi mpuuzi wewe. nimeshindwa kuipuka salamu hii kwani naishi katika jamii

salamu nyingine ni kama zile za kikrsto za bwana asifiwe, tumsifu yesu Kristo, Kristo, na zile za kiisilamu kama vile asalaamu aleikhum.

inakosekana mantiki ya salamu tuzitumiazo kwamba ni kwanini kwamfano tumsifu yesu kristo? kwa nini tusitakiane mema kama vile amani nk? mbona salamu aliyoitumia kristo enzi za uhai wake ilikuwa ni kwatakia awasalimiao amani? (amani iwenanyi/kwenu, amani ikaekwenu)

kwa nini tusalimiane salaamu kama vile shalomu tusizojua maana yake?

kumbuka salamu ni muhimu na sisi huwa yale tunayotakiwa na wezetu.

UPENDO DAIMA, AMANI, UPENDO NA MAFANIKIO VIWE KWAKO, nk, si salamu njema hizi?
najiuliza juu ya salamu zetu

2 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Bwana awe nanyiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!

Amos Msengi said...

Najitambulisha kwako kama mwana blogu mgeni kabisa katika safu hii ya kubadilishana mitazamo na kusaliti baadhi ya mawazo tuyaonayo hayana faida, ama yana nafasi ndogo katika dhana nzima ya uendeshaji wa maisha yetu ya kila siku.

Yesu alitumia salamu kama 'amani iwe kwenu' 'amani iwe nanyi' nk. Ni kweli waumini wa leo tumekuwa na salamu za aina nyingi, pamoja na hayo bado salamu hizi zinalengo moja la kumwinua YESU kama Bwana wa mabwana. Ikumbukwe kuwa Yesu asingesema " BWANA YESU ASIFIWE" au "BWANA ASIFIWE" au " TUMSIFU YESU KRISTO" kwa sababu yeye akikuwa MUNGU kamili na asingeuza wazifa wake kwa kumsifu ama kumwinua malaika au kiumbe mwingine. Yeye ni ALFA NA OMEGA, hakuna aliye juu yake.

Kuhusu shikamoo, ikumbukwe kuwa tunawaenzi wakoloni. Ukisoma historia ya biashara ya watumwa, utaona jinsi shikamoo ilivyotumiwa na watu wa jamii ya ASIA, na kwa kiarabu shikamoo ina maana ya "NIKO CHINI YA MIGUU YAKO". Hii ilitambulisha ukuu na mamlaka ya Sultani kuwa siku zote yuko juu. Salamu hii hata mimi hainipi amani kabisa, mara nyingi imetumiwa vibaya na baadhi ya watu ambao kisaikologia hupenda kuwa juu ya wengine na kuilazimisha shikamoo hata kama kiumri ni wadogo kuliko mtoa shikamoo.

Mfano utasikia mtu anaitikia 'marahaba' kutokana na mazoea wakati kasalimiwa....habari yako,....za sahizi...!.

Mtazamo wangu ungependelea salamu zisizo ambatana na shikamoo. Turudi kwenye dhima au maana ya salamu kuliko kuangalia utambuzi wa umri ili upewe shikamoo.

Pia ikumbukwe kuwa sio rahisi kwa kila mtu kumtambua umri wake kila unapokutana nao ili uamue kutoa shikamoo ama la!

"BWANA YESU ASIFIWE"