Thursday, July 1, 2010

sijui na mimi niweke nia ya ubunge!!

picha hii ilipigwa na kuwekwa pamoja na ujumbe huo


ilikuwa ni mwaka uliopita ilipotangazwa kuwa mwendashaji wa kijiwe hiki anajiandaa kuwa mbunge wa jimbo moja wapo bila kujua ni kupitia chama gani wala nini. na mwendeshaji huyo amehamia mikoani kwa muda mrefu sasa na jambo linaloweza kuonyesha ukweli fulani wa jambo hilo.

ujumbe huo uliwekwa na mtondo,lakini ni kweli nitaweka nia na kufanya mikakati ya kugombea? ni kweli ninachama cha siasa?/ lakini ni kweli mimi nataka kuingia ukumbini dodoma?je unadhani itakuwaje nikitinga kwenye jengo la Bunge?sijui kama kweli bado nina nia ya kuweka nia.labda unishauri

3 comments:

Mija Shija Sayi said...

kwa hayo maswali ulojiuliza naona ungevuta subira kwa kama miaka miwili hivi ili ujielewe kabisa umesimama upande gani. Unajua haya mambo ni rahisi kusema kama likiwa bado ni wazo tu, lakini ikishakuwa sasa ndio utekelezaji wenyewe unaona kabisa roho inavyoanza kudunda. Sasa kakaangu hebu anza chini ya hapo kwa japo ukatibu kata ili uanze kuwa sawa polepole.

Nakuaminia lakini.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

njoo chama changu!

chib said...

Nakubaliana na Mija, yaonekana hauko tayari kwa sasa, jipange vizuri, awamu nyingine uwe tayari kabisa. God bless