Saturday, August 21, 2010

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamalaaaaa! ugali na mandondo we umenikumbusha mbali na mate yanadondoka bila utaratibu na afadhasli hujaweka kisamvu na samaki au matembele hapo ningekuchuma mkuki..LOL

Maisara Wastara said...

Kamala hapo ni jela au?

Mbele said...

Nimeandika kiasi kuhusu masuala ya chakula na utamaduni, kwa mfano katika kitabu changu kimojawapo. Masuala haya yanafungamana.

Kuna vipengele vingi, kama vile imani na miiko kuhusu chakula, na pia taratibu za kuandaa na kula chakula. Tangu utotoni, tunafundishwa, kwa mfano, namna ya kunawa kabla ya kula, namna ya kukaa wakati wa kula, na kwamba tusiwe wachoyo.

Sisi wa-Matengo, tunafundishwa pia tangu utotoni kula mboga kwa namna ya kukuwezesha kumalizia ugali; si unafagia mboga na kubakiza ugali!

Kwenye hii picha, sisi wa-Matengo tutashangaa jinsi ugali ulivyopakuliwa na kuwekwa katika sahani bila kuumbwa vizuri uwe mviringo wa kupendeza kabisa, si hayo mapande yanayoonekana hapa, na wala si mviringo wenye mashimo, mabonde na vilima. Mwanamke wa ki-Matengo akileta mezani ugali kwa namna hii inayoonekana kwenye picha atasababisha sakata lisiloelezeka.

Nikija upande wa hayo maharagwe ni kwamba sisi wa-Matengo tunaweka maharage katika bakuli. Zamani walikuwa na vyombo maalum, vilivyotengezwa kwa udongo wa mfinyanzi, au kasha la aina fulani ya boga. Enzi zetu hizi, chombo cha kuwekea maharagwe ni bakuli tu. Mwanamke m-Matengo akithubutu kuleta maharage mezani katika kikombe au hiki kiplastiki kingine kinachoonekana katika hii picha, atasababisha sakata ambalo halielezeki.

Picha hii inanifikirisha, kwa maana kwamba najiuliza sasa kama kwenye makabila mengine suala la uandaaji na ulaji wa ugali na mboga likoje.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@ruhuwiko, DUHU, @maisara, kwa nini unauliza hivyo?

@mbele, kwetu sisi wahaya kuna mila miikona tamaduni nyiingi kuhusu chakula na ulaji, nitazijadili baadaye hapa kijiweni kwa kuwa ni ndefu

ila ughali sio utamaduni wetu kwa kweli hatujui kuupika kuupakua hata kuula kwakweli, ni chakula cha wakati wa shida uhayani

John Mwaipopo said...

upele umempata mwenye kucha. picha inafikirisha sana. nina rafiki yangu aliagana na maharage tulipomaliza form six (tena ni mhaya). mie ugali kwa mandondo 24/7, ilimradi maharage yasiungwe saaaana.

alamsiki binuur