Thursday, August 26, 2010

dunia ina nguvu nyingi za ziada!

inasemekana binadamu anatumia chini ya asilimia kumi ya uwezo wake wa akili. maajabu yoote haya ya sauti na picha kusafiri hewani, madubwana yanayofanya kazi kama binadamu, kuzalisha wanyama maabara nk, yote ni kwa kutumia akili za binadamu.

lakini tukijiuliza juu ya uchawi, ni kufanya mambo/vitu zaidi ya akili na mazowea? kushindwa kujua utokeaji wa mambo tunayoyaona (miujiza nk)?

vilipogundulika vioo, bunduki na hata ndege, baadhi ya mababu zenu waliamini ni uchawi!
utaalamu wa kitabibu wa kutibu watu kwa kulewesha akili (Hypnotism), ulizaniwa kuwa ni uchawi na wataalamu wa tiba hizo wengine walikimbia nchi zao, na walikuwa ni warumi, wagiriki, wamisiri nk

kuna watu wenye maono ya kuona mbali na bila shaka unafahamu mmojawa wao au wewe una maono pia je ni wachawi pia?

kwa hiyo duniani kuna nguvu nyingi sana za ziada na nguvu hizi uchukuliwa kwa njia tofauti. sisi kama binadamu tuna nguvu za akili, na hata za kiroho, watu wanajua nguvu zaona wana kanuni zao na huzitumia wapendavyo kufanya wayatakayo. kuna wenye uwezo wa kusaidia wengine, kutishia, kujinufaisha na hata kujipatia umaarufu, baadhi ya watu/jamii huamua kuwaita wachawi!

hizi ni nguvu tu za ziada alizonazo binadamu na hizitumia apendavyo japo zina malipo yake!!

itandelea... juu ya wanaologeka

2 comments:

emu-three said...

Mhhh, yah, kweli binadamu ana nguvu nyingi za ziada ambazo zipo `idle'(hazijawahi kutumika)!
Na kuunga mkono mkuu kuwa kama zingetumika vyema, hata huo uchawi wanaouamnini ungekuwa `dili' lakini wapiii! Wanautumia kuumizia watu. Nasikia kuna wanaowalimisha watu usiku...sasa kama wana uwezo huo kwanini hawaingii benki wakijichotea kilaini?
Yah, zipo nguvu za ziada lakini tumebetweka na kuiga nguvu za waliopita, hebu angalaia hata kuruka kwa ndege, mwendo wa magari yote hayo yalitokana na wale waliopita, sasa na sisi tukiamua kuzitumia akili zetu hizo zaidi tunaweza tukaendesha ungo kama usafiri rahisi tu....

SIMON KITURURU said...

Amen!