Tuesday, August 17, 2010

kuhusu uchawi, tupitie kwanza maoni haya;

emu-three said...
Uchawi ni imani ambayo lengo lake ni kudhuru, sidhanii unaweza kusema ngoma za kiafrika ni za kichawi vinginevyo ziwe zinachezwa na hawo wachawi kwa nia ya kudhuru.Ni vizuri usiamini kama anavyosema dada Yasinta, kwani ukiamini kitu kinakuwa na athari kwako

nyahbingi worrior. said...
mimi naweza sema,kabla ya mkoloni waafrika wengi tulitumia utamaduni wetu ambao baadaye wakaje sema ni uchawi.
kwa hiyo nyahbing anafananisha uchawi na tamaduni za kiafrika baada ya ukoloni kuja,

mjasiriamali said...
mimi nadhani uchawi ni kujua kitu ambacho wengine hawajui,mfano mimi na wewe kamala tuliwahi kuzungumza kuwa endapo unajua ''castomer care'' ya nguvu hao wasiojua wewe kwako huo ndo uchawi wa biashara.
kwa hiyo mjasiriamali anasema kwa mtizamo fulani finyu, uchawi au mchawi ni yule ajuaye zaidi ya wengine, au anayeamini uchawi ni yule mwenye mtizamo hasi


mjasiriamali said...
otherwise siamini uchawi wa eti kutumia ujanja ujanja usio na logic, never

Bennet said...
Huko vijijini ninakosafiri ndio imani hii inachukua nafasi kubwa sana, inafikia wakati mtu anashindwa kufanya mambo ya maendeleo kwa kuhofia kulogwa na wachawi, kwa upande wangu sina imani na uchawi

labda ni vizuri kutoamini katika uchawi, imani ni muhimu lakini kumbuka kuna imani, kuna uoga, unaweza dhani huamini uchawi, kumbe unauogopa uchawi jambo ambalo ni hatari. lakini kumbe uchawi ni mtizamo
ila kuna swali halikujibiwa, uliwahi kuloga au kulogwa au hata kutuhumiwa kuwa mchawi??

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

mimi sijawahi kuloga wala kulogwa na siamini kama mtu anaweza kumloga mwenzake.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

asante yasinta, ila unazua swali tena, huamini, lakini hujawahi kuwaona waliologwa na kuroga?? hata kwenye vyombo vya habari? au unwaona lakini huamini??