Thursday, August 19, 2010

nguvu hasi ni sehemu ya uchawi

kumbuka sisi kama binadamu ni nguvu, tunatengeneza nguvu na kutoa nguvu pia. mawazo yetu, maneno yetu na matendo yetu hutengeneza nguvu, nguvu hiyo yaweza kuwa hasi au chanya. ikiwa hasi basi ndo uchawi, ikiwa chanya ni amani, upendo na ni maendeleo pia au Mungu.

wale watu wa Mungu kama vile Jizaz, walikuwa wakitoa nguvu chanya tu. hata waliomtwanga makofi na vibao wakimtemea makoozi yao, aliwaombea msamaha huku akiwapa uhuru wa kuendela kumfanyia wayapendayo. kwa kifupi alihakikisha hatoi nguvu hasi na kwa hiyo alifikiri vizuri zaidi

hii ndivyo ilivyo au inavyopasa kuwa. lakini kwa sababu ya mifumo yetu yya kifikiri ilivyojazwa na nguvu hasi, sisi hutoa mambo hasi kuliko chanya na hivyo kuathiri wengine na kwa hiyo kwa njia moja au nyingine sisi tumewahi loga.

labda swali ni je, tufanye nini ili tusiloge na wala tusiloge? lakini je, kuhusu uchawi wa kupaa angani, kula maiti nk, vina ukweli au ni uzushi fulani tu??

tuonanaie next ijayo!

3 comments:

emu-three said...

Labda iwe hivyo kuwa hasi ni ubaya na ubaya tunaulinganisha na uchawi kwasababu dhana nzima ya uchawi ni kuharibu!

Anonymous said...

HII NI HABARI KUBWA ILA MSINIONE KAMA SIKWENDA SHULE UCHAWI UPO WACHAWI WAPO MIMI NIMEKWISHAWAONA KWA MACHO YANGU YA KUZALIWA HUYO MTU ALIKUWA ANATEMBEA HAJAKANYAGA CHINI HALAFU KUNA KAMA KIMVULI KIME MZUNGUKA.ILA KASORO MOJA MTU UKIONGELEA UCHAWI UNAONEKANA HUJAENDA SHULE,HUJASTAARABIKA,MJINGA,WATU WATAKUPUUZA

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@anony, mimi nauongelea sasa hii leo hapa, bado kuna meengi ya kuongelea. kama tunataka kuikoa jamii yetu, ni lazima tuwe wazi na kwa hiyo hapa tunaendelea na safari ya kuujadili uchawi na unakaribishwa kusema yoote uyafahamuyo au uliyowahi ona/sikia juu ya uchawi

Karibu