Tuesday, August 31, 2010

ni watu wa aina gani wanaologeka?

watu wanaologeka ni wale waoga na wajinga wa nguvu za maumbile wadhungu kwa asilimia 90, viongozi wa dini na watu wengine wanaoamini kwamba ndio wenye uwezo na nguvu za kuamua majaaliwa ya maisha yao na sio mwengineyo yote, kwa kiasi kikubwa hawalogeki wala nini

lakini waoga wa uwezo wa ziada walio nao wengine na wajinga a nguvu za maumbile hulogeka kiurahisi na ndio maana ni muhimu wakati mwingine mchawi kutoa vitisho kwanza ili aje kuroga!

pia wale wanaoshindwa kujua au kutofautisha kati ya miujiza. mazingaombwe na milango sita ya fahamu na nguvu nyingine za kimaumbile hulogeka kiurahisi pia na hivyo huamini na kuthibitisha juu ya uchawi na kuamini kuwa upo. wao nguvu hizi kwa kuwa hazielezeki kwa njia nyingine, huziita uchawi

kuna waliolelewa katika mazingira ya kauminishwa kuwa uchawi upo na unadhuru, hawa pia huweza kulogeka kumbuka akili zao zishaaminishwa hivyo

kuna wanaoishi kwa kutenda ubaya, hawa nguvu zao mbaya wanaozozitoa warudia na hivyo kuamini kuwa wanalogwa, kumbuka ile kanuni ya karma au action and re-action. matendo yetu, maneno yetu na mawazo huzalisha nguvu na nguvu hizi hazipotei, huturudia hata kama ni miaka 50 au maisha kwenye mwili mwingine na kwa hiyo huweza dhani wamelogwa

watu wenye tabia chafu, roho mbaya, nk ni rahisi kuhisi au kulalamika kuwa wamelogwa. ukitoa nguvu mbaya zitakurudia hizo hizo mbaya sana na kuamini kalogwa

lakini wengine wanaologeka ni wale wanaojihisi mikosi, nuksi, kukosa furaha, kuwa na hofu, kukata tamaa na wenye imani ya kutendewa ubaya na wengine!


itaendelea

6 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Endelea na hii mada kwani ni nzuri. Kuna padri mmoja wa Kikatoliki kule nyumbani alikuwa anawatoa mkuku wachawi au niseme wazee waliokuwa wakimzukia kanisani kwake wakiwa uchi. Katika mahubiri yake alikuwa akiwaambia watu kwamba si kila mtu anaweza kulogeka na yeye alikuwa haamini katika kulogwa na hivyo kujaribu kumloga ilikuwa ni kazi bure. Basi watu nao walianza kumwita mchawi na kudai kwamba alikuwa halogeki eti kwa vile uchawi wake ni wa kutoka mbali na Wasukuma walikuwa hawauelewi! Waliendelea kudai kwamba siku wakiuelewa basi atakwenda na maji.

Amelitumikia kanisa mpaka mwaka jana ndipo amestaafu na kurudi nyumbani kwao Uingereza.

chib said...

@ Masangu, ha ha haaa, naona hiyo ni njia nzuri ya kuwatishia walozi

Bennet said...

Kwa nini walozi hawafanyi vitu vizuri wao wanatishia kufanya mambo mabaya tu, mfano kuna njaa basi walete mavuno lukuki tuone kweli wao ni kiboko

emu-three said...

Dhana nzima ya uchawi ni kucheza na akili, kwa kuivuruga na kujenga `uwoga' na ndio dhamira ya hawo wanaoitwa wachawi.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Matondo hiyo hata mie kule kwetu nimeisikia kuwa eti "wazungu" hawalogeki. Ila mie siamini kwani kama kweli kama mtu analogeka basi nao wanaweza kulogeka si wtu tu kama sisi na pia wana imani. Kamala....kaazi kwelikweli

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ishu ya huyo padri wa matondo ni kama nilivyosema

@bennet kule mwanzoni nilioongelea aina ya uchawi nahuvyo sio sahihi kuwahukumu kwamba hawafanyi mambo mazuri au wanafanya mabaya pekee