Monday, August 23, 2010

Uchawi huko vichwani mwetu (VOODOO/VUDU)

Uchawi huko kichwani mwa anayelogwa na sio kwingineko. Ili ulogeke ni lazima kwanza hukubali/huamini au uwe na hofu kuwa unalogwa. Wengi wakitaka kumloga mtu, huakikisha analijua hilo na kuwa na hofu na hivyo wanaweza kumnuizia maneno au nguvu kwa kutanabana (kusema maneno kwa kutanabana) na hivyo kumloga mtu huyo

Lakini, angalizo ni kwamba, lazima mlogwaji ajue ya kwamba analogwa na kwa hiyo lazima awe ameingiliwa kisaikolojia kwa kupiwe vitisho, kupendwa kunafiki nk. Hayo ni lazima yamjengee hofo na hivyo hofu ni muhimu sana ili mlogaji aweze fanikiwa pamoja wa wasi wasi au mashaka.

Wengine hufu kwa kuamini katika uchawi haswa ulu uitwao VUDU (VOODOO) wenye asili ya afrika magharibi na kwa hiyo uchawi unauwa!

Kumbuka kuna mawazo na mawazo yanapoingia kweny hofu, huufanya mwili kubadilika kwa namna ambavyo tunaweza hata kufa

Bila hofu, kukosa matumaini na wasi wasi, uchawi hauwezikumdhuru yeyote na hivyo haufanyi kazi!1 na kwa hiyo ndiyo maana uchawi huwakamata watu Fulani Fulani zaidi!, Waafrika, Wa-Asia na wamerekani ya kati na kusini ndio ulogeka zaidi kutokana na mazingira na imani zao lakini umasikini na udogo wa sayansi na teknolojia husababisha mambo haya kuwepo kwa sana

Kali ni nchini Romania ambako mwaka 2002, wabunge walitaka uchawi utozwe kodi na kianzishwe chuo cha uchawi nchini humo!! Kali hii na waziri wa fedha wan chi hiyo alivunjika mguu baada ya kutangaza kodi kwa wachawi na wachawi wakajigamba kuwa hiyo ni adhabu kutoka kwao

itaendelea

3 comments:

Anonymous said...

kweli bw.kamala mwalimu wako munga ulimsomahasa.uchawi ulioko vichwani mwetu ni robo ya uchawi wote kwamaana ya uchawi kamili .ambapo hii robo ni hofu lakini robotatu inayobaki niuchawi kamili ktk uhalisia wake

emu-three said...

Kweli raha ya mchawi nikushinda, hata kama ushindi huo haukutokana na uchawi wake lakini atasema `mnaona' nyie nichezeeni tu'
Lakini hata mimi nikajiuliza kama mchawi anaweza kujigeuza paka, kama mchawi anawez kusafiri kwa ungo , kama mchawi anaweza kutembea mbele za watu tusimuuone, hatuoni hilo ni zinga la dili, kwanini tusiliboreshe tukaweza kuwaangamiza mafisadi wakati wapo kwenye kikao chao tunanafika tunasikiliza mwisho wa siku, mahakamani tuna ushahidi dhahiri.
Au vitani wote twajigeuza mipaka, nani uataua paka wasio na hatia, mmmmh, halafu mwaafiri na ungo, hatuhitaji ndege, fikiria Dar hii ingejaa ungo zinatembea hewani, Mumarekani angetuonea gele....jamani nyie wachawi mnapoteza nguvu zenu kuwangia watu bila faida, itafuteni faida ya kitaalamu...hili ni zinga la dili kwenu

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Natoka nje ya mada na naingia kwenye utani zaidi...

Wasukuma herufi r inatushinda (nimepiga kula leo)

Kule Mataranyirato herufi l inawapa shida (kura tumekura kurara je?)

Wachaga herufi ch ni ngoma nzito (Mzee wa Kiraracha - wananji wenzangu)

Wahaya - kwenye h wanaiondoa na isipotakiwa wanaiweka (Uchawi huko vichwani mwetu badala ya Uchawi UKO vichwani mwetu)

......

Kwingineko: Kwenye vitabu vitakatifu mfano pale Musa alipokuwa anajaribu kumshawishi Farao awaachie wana wa Israeli kulikuwa na bandika bandua ya kuamua nani zaidi kati ya Musa na wachawi wa Misri; na jamaa waliweza kuigiza karibu mifano yote aliyoifanya Musa. Biblia pia imejaa mifano mingi sana ya uchawi na wachawi - ambao hata hivyo ni chukizo kwa Bwana. Kwa hivyo kulingana na vitabu vingi vya dini, uchawi upo na wachawi wapo.

Lakini pia nakubali kwamba uchawi - kama vile Ujamaa enzi zile - ni imani! Ukiamini kwamba uchawi upo na unaishi katika jamii ya kichawi basi kila kitu katika maisha yako kitakuwa kimetawaliwa na imani hiyo - sawa tu na imani zingine mf. Ulokole.

Angalizo: yule kijana wangu aliyefariki wakati nikiwa nyumbani mwezi wa sita inasemekana bado yupo na anafukuza watu pale kijijini. Hata siku moja amewazukia wanafunzi na walimu pale shuleni kijijini na kuanza kuwafukuza mpaka shule ikabidi ifungwe. Watu walikuwa hawajidamki asubuhi au kutembea nyakati za jioni wakiogopa kukutana naye. Wale jasiri wakijaribu kumsogelea eti anatoweka. Mazingaombwe ya dunia!