Monday, August 16, 2010

uchawi!

baadhi ya tamaduni za kiafrika hufananishwa na uchawi au huitwa uchawi
sasa ni wakati mwafaka wa blogu hii kujadili suala lililotia fora katika jamii nyingi za kiafrika na hata kidhungu, sasa tunajadili suala la uchawi eti kwa ufahamu wako, uchawi ninini?? unaamini kuna uchawi?? je uliwahi kuloga au kulogwa kwa njia moja au nyingine?? je Mchawi anafananaje? lakini je tunawezaje kuepuka uchawi (yaani kuloga na kulogwa)?

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

siamini kabisa mamboya uchawi!!!!

emu-three said...

Uchawi ni imani ambayo lengo lake ni kudhuru, sidhanii unaweza kusema ngoma za kiafrika ni za kichawi vinginevyo ziwe zinachezwa na hawo wachawi kwa nia ya kudhuru.
Ni vizuri usiamini kama anavyosema dada Yasinta, kwani ukiamini kitu kinakuwa na athari kwako

nyahbingi worrior. said...

mimi naweza sema,kabla ya mkoloni waafrika wengi tulitumia utamaduni wetu ambao baadaye wakaje sema ni uchawi.

mjasiriamali said...

mimi nadhani uchawi ni kujua kitu ambacho wengine hawajui,mfano mimi na wewe kamala tuliwahi kuzungumza kuwa endapo unajua ''castomer care'' ya nguvu hao wasiojua wewe kwako huo ndo uchawi wa biashara.
Johns

mjasiriamali said...

otherwise siamini uchawi wa eti kutumia ujanja ujanja usio na logic, never

Bennet said...

Huko vijijini ninakosafiri ndio imani hii inachukua nafasi kubwa sana, inafikia wakati mtu anashindwa kufanya mambo ya maendeleo kwa kuhofia kulogwa na wachawi, kwa upande wangu sina imani na uchawi