Wednesday, August 11, 2010

yallyojadiliwa katika mkutano wetu dar

Mkutano wetu ulianza saa tatu na nusu usiku, siku ya jumamosi tarehe 7 mwezi wa nane. Tulilazimika kukutana muda huo kutokana na baadhi ya wajumbe kuwa na safarikesho yake asubuhi, lakini pia kukamilisha adhma hii. Basi saa tatu na robo hivi tukakutana hotel ya layoni (lion) iliyoko sinza.

Bila hata kujitambulisha, tulionana na kutambuana kwa nyuso na hivyo kuanza mazungumzo moja kwa moja tukaja kugundua baadaye kuwa hatukujitambulisha mwanzoni. Kwa kifupi tuliongelea maisha yetu, maisha ya vijana na hadaa zilizojaa katika vyombo vya habari na kila pahala vitu tunavyovipromoti na umuhimu, badala ya kupromot elimu kwanza

Lakini swala likaja juu ya elimu yetu na aina ya elimu bongo,na umuhimu wa elimu hiyo.prof alisisitiza mno juu ya kujitambua,alitoa mfano jinsi alivyopelekwa kusoma marekani, akiagizwa na Nyerere kwenda kuhemea na kurudisha chakula, kwa hiyo akaenda kusoma ili kurudisha elimu nyumbani. Anasema aliporudi bongo, alikuja navitabu vingi sana, ila jamii ya bongo wakiwemo wasomi walimshangaa kwamba kaja na lundo la vitabu badalaya ya kuja na magari kadhaa.

Prof aliongelea juu ya wazee wetu /mababu zetu na elimu zao jinsi zilivyokuwa muhimu na zinaogelea mazingira halisi, alitoa mfano wa misemo ya wahaya na busara ndani mwake,kwa mfano mwanamke akimwambia mumewe kuwa, jinsi ndizi ilivyodondoka, mh ni bora asiende anakotaka kwenda. Mume akibisha, wakati mwingine huenda na mambo yasiende vizuri na hivyo kuwa na fundisho la kumheshimu kila mmoja badala ya kuwadharau watu kwa ubaguzi wowote uwao ule.

Pia alisemea juu ya misemo, nyimbo na majigambo yaliyokuwa na elimu, maarifa na ujuzi mwingineo.lakini prof. Mbelle anasema elimu ya sasa inasikitisha, ambako waalimu na hata waadhiri wako bize na miradi binafsi. Kwa hiyo elimu ya kujitambua ni muhimu sana
kabla ya mkutano huo tulipata wasaa wa kuongea na yasinta kwa njia ya simu na faith mtanga

KUHUSU BLOGU ZETU

Tuliaza juu ya u-slow wa mtandao. Prof. Mbelle alishangaa sana juu ya mitandao yetu inavyokuwa slow ile mbaya naakasema kwa kweli ni vigumu kuweka / kutundika picha nakwa hili aliungana na mtanzania-mmarekani mwingine (Matondo) kuongelea juu ya jambo hili la U-slow wa mtandao na kuwaonea huruma wana blogu wa Bongo

Lakini pia alishangaa jinsi gharama za internet hapa nchini zillivyokuwa juu na hivyo kuwa ngumu kwa watanzania kublogu na kutembelea blogu nyingenezo. Tuliongelea pia juu ya mbinu za uandishi katika blogu zetu, tuliongelea changamoto za uandishi wa makala ndeefu bloguni zinavoboa kwamba watu wengi hupenda kusoma vimakala vifupi fupi na pia ni muhimu kutundika vitu vipya bloguni mara kwa mara na sio mara moja kwa wiki au kwa wiki mbili ili kufanya blogu zetu kuwa active

Faida na mbinu nyinginezo za kublogu tulikutana na changamoto juu ya blogu za udakuna zisizo za udaku, kuwa blogu ni shule na hapa ukakumbukwa msemo wa Mubelwa badio kuwa ‘blogu ni shule,wafundishao ndio wafundishwao’

Tuligundua pia kuwa blogu zinatujengea uhusiano na undugu mpya lakini pia kwamba mtandao (networking) ni muhimu ili blogu zetu ziweze kuwa na wasomaji wengi, kwamba ukiweka link ya blogu nyingine katika blogu yako ni muhimu kwako na kwa hao wengine pia.

Iligundulika kuwa blogu zetu ni muhimu pia ikizingatiwa kuwa kuna watu wana print baadhi ya machapisho ya blogu zetu na kuyatumia huko walipo katika mafunzo mbali mbali au kuyasambaza wakiyasoma na kuburudika na hivyo mchango wetu ni mkubwa na muhimu katika jamii

Suala la kutoegemea upande wowote (liberalism) liliongelwa zaidi kwamba mblogu (blogger) anapokuwa liberal katika maandishi yake, hupata changamoto nyingi na kujifunza zaidi kuliko kushambuliwa na kubishana tu

Liliongelewa suala la uchumi wa bloggers kupitia blogu zetu na kwamba elimu inahitajika zaidi hapa juu ya vileta uchumi kama ads,lulu,adverts nk

Tuliongelea juu ya kubadili fikra, kusaidiana na kuwa na umoja. Mfano ulitolewa kwa mtanzania anayeishi killwa au kanyigo, akianzisha blogu yake, tunamsaidiaje aweze kufahamia, kujiamini na au kutembelewa? Tulionngelea pia jamii zetu au wasomaji wetu, lakini pia watanzania wanashindwa kutembelea blogu zetu kwa sababu ya uelewa, ukosefu wa mtandao na gharama kubwa za mtandao

Bwana kamala alielezea uhuru wa kutoa maoni kwa njia ya blogu bila kulazimika kupitia njia gani gani sijui, kwamba unaandika vile upendavyo bila kubwanwa na mtu au upande wowote ule

Kwa kifupi hayo ndiyo yaliyojadiliwa, ila kuna changamoto ya swali tulilojiuliza sisi kama mabloggers, itatundikwa kesho ili tuijadili, mkutano wetu ulifungwa saa tano na dakika hamsini usiku, kila mtu akaelekea alikotoka. Tulikukwa na wakati mzuri sana kwa kweli, vivizuri kukutana kama tulivyokutana

3 comments:

danie said...

nmekukubali kiongozi kweli ua ideas zinaendena na mwenendo wa vijana,
endeleza limbi la mawazo endelevu ili kuleta mwamuko wa kweli wa kizalendo kwa vijana,
taifa ni letu lazima tulijali

its
Danstan Kaijage

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

karibu sana danie, waihyuka nokubaasa kukomenti, olaijage nkeibala lwaaywe

Wachumi said...

poa sana!