Wednesday, September 22, 2010

biblia, kitabu cha ajabu jamani!


hivi ushawahi kujiuliza ni vitabu gani dunia hii vyenye kukanganya, kufarahisha na kuburudusha huku vikiwa vipya kila siku??

vitabu vya dini au vye habari za kiroho navyo huitwa vitakatifu kama vile koran, bavaghadGita, granth sahib/adhi granth na hata biblia ni vitabu vya aina yake.

niongelee biblia kwani wengi wetu hapa twaijua hiyo tu au hiyo zaidi. biblia ni kitabu kipya always, kinavutia na hakikatishi tamaa hata kidogo. huwezi kusoma verse fulani na ukasema hamna haja ya kuendelee kusoma kwani hapa niliisha pasoma, hapana, utasoma mpaka uchoke

ni biblia hiyo hiyo inayosababisha majina fualni kutumia ulimwenguni na hivyo kukuta majina yakijirudia rudia utadhani hamna Mengine na hivyo kila mzazi humwita mwanae jina fualani mradi liko kwenye bible hata kama hajui maana yake

wengine biblia hutumika kama irizi na ndia maana siku hizi zinatengenezwa ndogo ili mtu aweze kuibeba mfukoni, kwapana na kulala nayo chini ya mto

ni kitabu cha ajabu, biblia, changamto ni kwamba wengi wanaipenda lakini kamwe hawaiishi, bubakia kutamba wanavyojua kuisoma, kuinunua, kuibebe nk lakini maneno yao , matendo na hata mawazo mara nyingi hufanya kile kilichokinyume na biblia!!

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Biblia Kiboko , si unacheki inavyosaidia watu kuchanganyikiwa, makanisa kibao ambayo ni dalili kuwa haieleweki,.........?

Na ukifuatilia historia ya jinsi ilivyoandikwa IJULIKANAYO ndio kabisaa unaweza kukwazika na dini yako kama weye ni Mkristo.:-(

emu-three said...

Ndio maana vitabu vitakatifu vinaitwa maneno ya mungu, ukiyatumia vyema yatakusaidia ukiyatumia vibaya....we mwenyewe waona!