Monday, September 27, 2010

biblia na chimbuko la dini

tukumbuke kuwa yesu Kristo hakuwahi kuandika biblia na vitabu vya biblia (agano jipya) viliandikwa baada ya kuwa yesu ameondoka. kwa hiyo watu tunasoma biblia tukimtafuta Mungu bila kuilewa na hapo ndipo ilipo chanzo cha dini

kwa mfano ubatizo, tunaona ukiwa utamaduni wa waebrania/wayuda. sasa yesu anabatizwa lakini Yohana anasema kuna asiyebatiza kwa maji bali kwa roho na kweli

nauliwa maswali kama nimeisha mbatiza mwanagu kipenzi ila mimi sielewi sana swali hilo. sasa tunaona ukriisto kama wakatoliki na KKKT wakibatiza kwa tujimaji kidogo, wapentekoste wanataka mtu azamishwe kama ilivyokuwa wakati wa Yesu, na wengine huzama jumla, huliwa na mambo nk, lakini wengine sasa wanataka maji ya kubatizia yatoke kwenye mto unaoaminika kuwa ndiko aliko batizwa yesu yaani mto yordan / jordan

hiki ni chanzo cha dini lukuki, kutokuelewa biblia

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Imani ni ukichaa kidogo kama tu KUPENDA mtu!:-(

Na kwa imani WASABATO na WAKATOLIKI ingawa wengine BIBLIA inawaambia jumamosi ndio siku bomba , wengine huamini kwa kudai ni JUMAPILI kushusha sala na kumsifia MUNGU kama vile anahitaji kweli kusifiwa na wanadamu NDIO SIKU BOMBA ,...hasa ukizingatia isemekavyo MUNGU ndiye muwezesha yote.:-(

Na kwaimani labda kitabu cha JUMA na ROZA kinaweza kuwaanzishia watu dini.:-(

Ni mtazamo wakati nawaza ya BIBLIA!:-(

Anonymous said...

Kabla ya Biblia kulikuwepo na dini!