Friday, September 17, 2010

blogu hii yajikuta ikijadili siasa!

ni kawaida ya blogu hii kukwepa na kutokujiingiza katika masuala ya kisiasa, ni baada yakutumia pepe juu ya ubora wa Dr slaa sasa blogu hii inajikuta ikijadili mambo ya politics japo sio lengo lake na haikuwahi kukusudia hilo, sasa basi tusome ujumbe kutoka kwa mchangiaji na majibu yake.........

Matondo Nzuzullima said..

Nina wasiwasi sana na "ukombozi" huu wa kutegemea "masihi" mmoja. Watu wamesahau kwamba alikuweko mtu mmoja akiitwa Mrema (na NCCR Mageuzi ya akina Mabere Marando na Makongoro Nyerere) ambaye alikuwa akibebwa na gari lake kusukumwa kila alikoenda. Sijui leo yuko wapi.

Halafu akaja Mchungaji Mtikila na siasa zake za magabacholi. Moto ukawaka, watu wakavua mashati, mioyo ikadunda na midundiko ikachezwa. Sijui leo yuko wapi.

Halafu wakaja ngangari wa CUF na Lipumba wao na Maalim. Nao jua lao likachomoza, hiloooo tukaliona, saa sita ikaingia na hatimaye jioni yao ikafika. Leo hii Lipumba yupo kama hayupo.

Asubuhi ya Dr. Slaa ndiyo hii imeshafika. Mimi hata hivyo sina matumaini sana kwa sababu mabadiliko tunayohitaji ni ya kimfumo hasa na siyo ya kutegemea mtu mmoja mchapakazi mwenye bashasha. Siwajui sana Chadema lakini sijui kama Dr. Slaa ana wafuasi wa kweli wanaoamini kile anachokiamini kwa asilimia 100. Historia inatuonyesha kwamba bila wafuasi wa kweli, ni vigumu sana kwa mtu mmoja kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii. Kamuulize Nyerere atakwambia. Yeye alikuwa akiimba Ujamaa na Kujitegemea wakati wenzake waliomzunguka wakijibeparisha (Rejea hapa: http://matondo.blogspot.com/2009/10/mwalimu-nyerere-na-jangwa-lake-la.html)

Japo email ya huyu mdau - ambayo imeenea mtandaoni - inamchora Dr. Slaa kama Musa wetu - bila wafuasi wa kweli na mshikamano wa dhati na umma ni kazi bure. Na mashabiki wake inabidi wawe tayari kuyakabili maluweluwe yatakayowapata baada ya uchaguzi. Na baada ya uchaguzi huu naamini wataanza kutafuta nyota nyingine inayong'ara zaidi. Natumaini pengine atakuwa Mh. Zitto.

Mabadiliko yameanza kutokea lakini ni ya polepole na mimi naamini kwamba bado safari ni ndefu kidogo kwa wapinzani kuweza kukifikia kilele. Ili kufikia azma hiyo inabidi wasiwe tu wanasubiri wakati wa uchaguzi ndipo wanakurupuka kutoka usingizini huku wakiweka matumaini yao yote kwa "Musa" mmoja tu mshika kurunzi! Ukombozi wa kweli wa wanyonge ni kazi ya wote na ni kazi ya masaa yote 24, kutokea Jumatatu mpaka Jumapili; na mwezi wa kwanza mpaka wa kumi na mbili wa KILA mwaka!!!


nami nikamjibu hivi

Blogger kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@matondo, naamini daima tunahitaji mtu mmoja wa kwanza wa kuongoza au wa kushika tochi na wengine watafuatia tu, siamini kama ni Slaa pekee, wapo wengi hata wengine ndani ya CCM na vyama vingine ambao ni wakombozi wa kweli lakini kwa sasa ni zamu ya DR slaa kuongoza mashambulizi

binafsi sina upande kivyama ila napenda tanzania iliyo bora kwa wote


wewe Anony kuna vitu viwili umesahau kwamba labda hata wabunge woote wa chadema ni wachagga, lakini pia hata mchaga anasifa za kuikomboa nchi kama ataona ni yeye na wachaga wenzake wanaoweza kuikomboa tanzania

ila sasa CCM nayo ni ya masikini au?


angalizo hapa ni kwamba mimi sio mwanasiasa, sipendelei saana kuongelea siasa ila nimejikuta nikifanya hivi kwa sababu naishi kwenye jamii ya siasa, na mimi kwa vyovyote ni muathirika wa siasa na pia kwenye ushindani, ni lazima niangalie lakini pia nijikute nashabikia upande fualni!


Delete

11 comments:

chib said...

Siasa haikwepeki sasa hivi

Fadhy Mtanga said...

mie najaribu kuikwepa siasa lakini kama asemavyo kaka Chib yenyewe haikwepeki.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndio, na nilazima uonyeshe upande, interesting inajulikana tu mtu critical yuko upande gani!!

John Mwaipopo said...

siasa ingekuwa silaha ya maangamizi wote tushaangamia maana haikwepeki. na ulichofanya wewe ni kukopi na kupesti. usijali. kinachovutia zaidi katika siasa za mwaka huu ni kuwa kuna upande mmoja una miundombinu kibao ya kukusanya watu kwenye mikutano yao. watu hata hukodishiwa malori ili kujaa mikutanoni. kuna upande mwingine watu huudhuria kwa gharama zao wenyewe

Mzee wa Changamoto said...

Bado siamini maamuzi ya Dr Slaa kugombea uRais. Nadhani angezunguka nchi nzima akipiga kampezi za watu kuchagua wabunge wa upinzani.
Hivi hawa wana nini kwenye ngazi ya KAYA ambacho tunaweza kujivunia kuwa wakipata madaraka WATAFANIKISHA utekelezaji wa sera walizonazo?
Kwani hata SLAA AKISHINDA LEO WAKATI 90% YA WABUNGE NI WANA-CCM, UNADHANI ATAMUADHIBU NANI? ATATUMIA KURA GANI AMA SHERIA GANI ISIYOPITA BUNGENI KUWAADHIBU ALIOSEMA WANAIIBIA SERIKALI?
Pengine ni wakati wa sasa watu kutambua kuwa tunahitaji miaka 5 ijayo kujijenga katika ngazi muhimu za chini kabla ya kuanza omba ngazi za juu.
Hivi nchi hata iongozwe na MASIA anayetawala ki-demokrasia, unadhani itafanikiwa kama asilimia 98 ya watendaji ni WAPINZANI WAKE tena wasiopenda kuona anafanikiwa?
Nadhani Slaa anachotakiwa kufanya ni kukubali kushindwa kisha kutumia misingi waliyojenga kuzunguka nchini bila kuchoka kujenga ngazi za chini.
Japo hili haliwezekani kirahisi kwa kuwa uchaguzi hautafanyika mpaka miaka 5 ijayo. Nilitamani kama ungekuwa unafanyika miaka 2.5 ijayo kama nilivyandika (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/07/nionavyo-mimi-uchaguzi-wa-rais-na.html)
Uchaguzi ungekuwa unafanyika katikati ya muhula, Slaa na wenzake wangeendelea na kampeni kwa miaka 2.5 kisha kuhakikisha wabunge na watendaji wa kata wanabadilika kisha "wamchachafye" rais kuhakikisha anatekeleza ahadi na kama anakamilisha ahadi vema zikawa zinapingwa na wabunge, apelekewe wabunge watakaoms-sapoti ili kuwafaa wananchi.

Anonymous said...

hivi kwa nini watanzania mlio ughaibuni mna wasiwasi sana na mabadiliko ya utawala? mubelwa you are singing the same song a friend of mine in Oregon is singing. 'slaa akubali kushindwa', nani keshatangaza matokeo. the ballot box will speak loudly and clearly. nani anashindwa nani hashindi ni kazi ya tume hebu na tuiamini.

slaa hataweza kuongoza ikiwa wabunge hatakuwa nao. nani kasema watu wanampenda slaa tu ila hawawapendi wabunge waliosimama kwa upinzani?

nadhani mnaangalia historia ya mwaka 1995. mnayoyaona nasi tunayaona tena sisi tupo hapa hapa. there are 6000000 new voters who have never voted since they were born.nani anajua watapiga kura kwa nani?

nadhani suala la nani atashinda na nani atashindwa lina wahusika wake. leo si vema kuwasemea watanzania kuwa slaa akubali kushindwa au ccm itapata wabunge 98%. hivi inakuwaje urais unampigia slaa ubunge unampigia ccm?

mlioamua kuishi nje mtuachie tanzania yetu.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...
This comment has been removed by the author.
Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Anony @ September 19, 2010 12:49 PM

"mlioamua kuishi nje mtuachie tanzania yetu"

Hatuwezi kuwaachia kwani hata sisi ni Tanzania yetu na tunaipenda sana; na tunashiriki katika ujenzi na maendeleo yake kwa hali na mali. Tuko huku tu kubeba maboksi lakini mioyo, utu na utambulisho wetu viko nyumbani Tanzania. Naamini kwamba hii ni haki yetu ambayo haitatishwa kwa vile tu eti "tumeamua kuishi nje!"

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

tayari ushakuwa mwanasiasa japo ile kadi yako ushawapa mchwa wakafanya sherehe na kucheza 'engoma ya abhateshweka'....lol!

Matondo, now you are talking...lol!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mzee wa changamoto labda na matondo, maneno yenu kama alivyosema anony, yanaonyesha kuwa ughaibuni ni tatizo la kutokuelewa mabadiliko. kwa taarifa yenu mabadiliko ya kisiasa yaliyojiokeza tz ni makubwa na huwezi kuyasemea ukiwa nje ya tz kwani vyombo vingi vya habari vya hapap vina bias kwa hiyo mtizamo wenu kuwa CCm ina wabunge wengi ni potofu sana hata kabla ya kura kupigwa
unoongelea sheia, ni kwamba zipo ila hazina watekelezaji na kumbuka rais wa TZ kikatiba ana mamlaka ya ajabu mnmo

John Mwaipopo said...

give us a break! nyote mnaodhani tanzania bado kufanya mabadiliko your wish will be granted lakini haikatazi kuona kuwa kuna sehemu ya watanzania wanaotaka mabadiliko ya kweli, within or outside the vanguard party. atashinda mumtakaye lakini tuwaache watanzania waseme october 31. hata kama wanaotaka mabadiliko wataambulia robo, robo ni namba ya kujua watu wanataka nini?

leo tunasema bado, tayari itakuja lini? leo ni kama siku zingine zote za tayari. wakati nyerere anawania uhuru wa nchi hii, watawala walitumia neno 'bado' mpaka mwenyewe akaandika 'we are tired of these bados"