Friday, September 3, 2010

kulogwa na maisha kutokuwa na maana

kumbuka uwa uchawi kwa wakati mwingine au ile hali ya kuhisi umelogwa, uambatana na hali ya maumivu ya kihisia na hivyo tunaweza ugua maradhi ambayo hata tukienda hospitali tunaambiwa ugonjwa haupatikani au tunatumia dawa bila kupona.

kwa mfano ukimdanganya ustaadhi baada ya msosi kuwa umemlisha nyama ya nguruwe, anaweza kutapika kwani hisia zake kupitia akili zake zimefundishwa kuwa nguruwe ni haramu na hivyo ukimdanganya atakukubalia atatapika tu kwa kuwa hisia zake zinaamini hivyo

lakini watu hapata maumivu ya kihisia na kuamini wamelogwa na hivyo kujiloga//logeka. vitu kama kukata tamaa, hofu, hasira, simanzi nk, huweza kuleta imani ya kulogwa endapo mhusika hatapata usaidizi wa kisaikolojia na hivyo kuona maisha hayana maana tena.

watu wengi hapata maradhi yasiyojulikana au yasiyotibika hospitalini kama vile, maumivu nyuma ya shingo vidonda bya tumbo, kizungu zungu, maumivu ya kichwa, kukosa choo, uchovu wa muda wote nk

haya yote kuna uhusiano kati ya mwili na hisia zetu

next ijayo tutaona juu ya uchawi na umasikini

No comments: