Thursday, September 30, 2010

nakumbuka mapigano ya dini udogoni!!


ndugu zangu binadamu anapenda kubaguana na ndio maana binadamu wa kikoloni walijitahidi kueneza ubaguzi wa kufa mtu kwa watumwa wao. kuna ubaguzi wa rangi, kabila, taifa, bara, nchi, pua, kimo, jinsia, uelewa nk. nk, nk

sasa nakumbuka mafundisho ya dini yangu udogoni yalivyonisisitiza kubagua dini nyingine kwamba woote wanamfuata shetani (yule jamaa anayetisha) isipokuwa dini yangu pekee ndo sahihi basi tulitukanana kati ya wakatoliki na waluteri kwa kihaya chetu ngoma nzito ilikuwa kati ya wakristo na waisilamu.

siku moja tukiwa tunaelekea chekechea ya dini, tulikatiza msikitini na kukuta watoto wenzetu wamemaliza madrassa, tulipigana mawe, viboko, makofi nk, ilikuwa ni kati ya waisilamu na wakristo.


baada ya kuachiana ngewe za kutosha na vjana wa kiisilamu, ngoma ikawa ni kati ya waprotestant na wakatoliki, wewe piganaaa, then ngoma ikawa ni matusi juu ya nani hashiriki na anayeshiriki ile iitwayo meza bwana
inashangaza, ubaguzi na utengano katika umri mdogo ule! DINI n mapigano huku zote umtafuta MUNGU wa upendo na amani

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Neno la leo ni neno kweli! Lakini hata tufanye nini wote kila kitu tufanyacho, tuombacho nk, nk yaani hata ziwe dini malaki na malaki wote tuna mwomba Mungu MMOJA tu ha kama kuna dini tofouti sijui ngapi lakini wote tunamwomba Mumngu mmoja tu, hata kama wewe unaabudu mti lakini maombi yako yanakwenda kwa mingu yuleyule nimependa nukuu hii "DINI n mapigano huku zote umtafuta MUNGU wa upendo na amani"

emu-three said...

Swali kubwa la kujiuliza ni je `hayo yakupigana ndivyo kweli maandishi yamesema hivyo, ndivyo kweli mwenyezimungu katuamurisha hivyo, au ni `chuki zetu binafsi' tunazipandikiza katika mgongo wa dini..?

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

duh!

na yanaendelea mpaka sasa...unadhani yamekwisha?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@enu-three, umesoma agano la kale uakona vita ya kimungu???

Mbele said...

Hii makala yako inasisimua sana. Umeonyesha vizuri ujinga tunaouendekeza duniani kwa kisingizio cha dini.

Makala yako imenikumbusha kaujumbe nilikowahi kuandika kuhusu suala hili. Bofya hapa.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Binadamu!