Saturday, September 11, 2010

nimefagilia hii koment juu ya kukojoa popote

Hapo zamani za kale kila sehemu ilikuwa choo kasoro tu pango unalolala mwenyewe. Choo kwa tafsiri ya siku hizi ni kitu kipya kwa hiyo ndio maana si jambo ambalo Binadamu anayezaliwa tu na kuanza kujinyea na kujikojolea analo kwenye DNA na ni lazima linamuathiri kinamna. Kwa kuwa labda kukojoa chooni na kujifunza kula kwa kijiko ni vitu mtu ajifunzavyo tu kwa kuwa kukata tonge kwa mkono mtupu inawezekana.

Kwa hiyo kuna uwezekano kirahisishacho wanaume kugeuza wakati wowote ni wakati wa chai na mahali popote kama unaweza kuficha kirungu ni pa kukojolea ni swala la Kibaolojia, Kisaikolojia na ni kwa kuwa inawezekana.

Na sababu za wanawake kutovua chupi adharani ili wakojoe ni sababu za KIBAOLOJIA, Kisaikolojia na sababu za kuepusha kuwapandisha watu munkari uwezao kupandisha njema ashki kwa kushuhudia tu mwanamke anateremsha chupi chini kidogo hata kuzidi ya kusema Wanawake wao hawakojoi hadharani kwa kuwa wamefundwa wakafundika.:-(

NIMEACHA!:-(

No comments: