Saturday, September 4, 2010

Nimeona mjadala wa vijana TBC name naona ni bora nitoe maoni yangu japo kwa uchache juu ya yaliyojadiliwa

Hasa hoja ya kuwa vijana hawana experience na kwa hiyo hawafai kuongoza. Kuna jamaa aliwahi sema kuwa experience is the teacher for the fools, hivi ni kweli tunahitaji uzoefu ili tuweze kuongoza? Sidhani kama ni kweli

Lakini hoja nyingine ni wazee wetu pamoja na experiences zao, wametupeleka wapi? Mbona taifa letu haliishiwi na matatizo tuliyonayo? Mbona ufisadi unazidi kutudidimiza na kutupoteza na kutupeleka pabaya na matatizo mengine? Mbona maadui wale wa enzi wanazidi kuongezeka? Ni kweli tunahitaji experiences za wazee hawa au tunahitaji mbinu mpya na njia mpya za ufanyaji mambo ili kukabiliana na changamoto tulizonazo na njia hizo mpya si zinatoka kwa vijana zaidi?
Lakini tuangalie hata uhalisia wa ulimwengu wetu huu na maisha tunayoishi, mabadiliko yoote yanaletwa na vijana. Angalia ICTs, kwenye mitandao vitu kama face book, twitter, online forums nan hata simu za mkononi, mabadiliko yoote yameletwa na vijana na huweza kuendelezwa na vijana zaidi kuliko lika lolote lile.

Mapinduzi mengi ya kiuchumi na siasa safi duniani huletwa na vijana zaidi. Angalia marekani walivyokuwa na ushiriki wavijana, hata uingereza wamelazimika kuchagua viongozi ambao wanaumri mdogo zaidi kwani ndio wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za ulimwengu wetu huu kuliko lika linginelo
Hata Tanzania, nyerere asingeweza kufanya aliyoyafanya kama angesubilia kuzeeka kwani tunashuhudia wenyewe alivyozeeka na kuamua kuachia ngzi huku mambo yakiwa yanaenda kivinigine

La muhimu kwa vijana ni kujitambua, kujua sisi ninani, tunatoka wapi na tunaenda wapi, ni kujua kuwa ujana ni wakati muhimu sana wa kujikomboa na kukomboa jamii yetu na hivyo tuishi maisha tuliyonayo ya sasa kwani kesho haipo. Tusisubili kuzeeka eti tupate uzoefu ulimwengu unabadilika na hivyo uzoefu hautupeleki popote pale
Vijana walioko vyuoni hawashindwi kugombea kwani wanaweza tu kuwakilisha wananchi wakiwa masomoni au hata kuhairisha masoma kwanza na kuitumiakia jamii yao, kwa nini kugangania shule wakati unanafasi ya kutumikia jamii?
Kwanini vijana wanaosoma U-Dom wasigombee udiwani na ubunge wa pale Dodoma walipo karibu na jamii zao au wanaosoma UD wasigombee ubunge wa Ubungo na udiwani wakijua ni karibu na shule na nikaribu wananchi wao??
Sometimes we learn through mistakes, but if we wait for mistake to learn through them, we shall die unlearned , so we have to learn from the mistakes of the others.
Angalia hata mitume na manabii wa dini zote walikuwa vijana na sio wazee na walipingwa sana na wazee japo walifanikisha, kwa hiyo hii ni sruggle

I remain
Kamala Lutatinisibwa

No comments: