Monday, September 20, 2010

politics; KKKT, serikali: hamna fedha za kutosha!!!

wapenzi wasomaji, leo naendeleza siasa kidogo na maamuzi yetu. jumamosi iliyopita nilihidhulia sikukuu ya vijana na askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) hapa mjini bukoba. viongozi wa kanisa hilo akiwemo askofu, katibu Mkuuu na mchungaji wa vijana walilalamikia ukoseu wa fedha ili kufanikisha siku hiyo na miradi mingine

binafsi sikuona kama wako kivijana zaidi japo ni sikukuu ya vijana na askofu na labda wako kivijana wa zamani. ishu ni kulalamikia upungufu wa pesa badala ya kuwa wabunifu na siku hiyo ikawa kivijana zaidi. kila aliyesimama kuongea alilalamikia ukosefu wa fedha na bila shaka umasikini wa taifa hili

na siasa ni hivyo hivyo, serikali itakwambia kuwa hatuna fedha za miradi ya waliowengi na kwamba nchi yetu ni masikini sana.! inashangaza jamani. hivi kwa nini fedha hazipatikani kwa ajili ya miradi ya waliowengi lakini zinapatikana kwa anasa namaisha ya waliowachanche??

kwenye siasa, viongozi anatembelea magari ya kifahali ya kuanzia milioni miambili na kuendelea. wanalipwa mishahara ya ajabu na maurupurupu ya nguvu, wanaishi kwenye majumba ya anasa, watoto wao wanasoma shule za gharama sana lakini likija suala la miradi ya wengi kama vile kuboresha elimu, afya, maji, umeme, nk, hamna fedha

hili pia lilinishangaza katika siku hiyo ya vijana na askofu ya KKKT Bukoba, hamna fedha,lakini mbona mishahara ya viongozi wa juu haikosekani daima? mbona wanaishi kwenye nyumba za kifahali na maisha ya gharama?? askofu anatembelea shangingi na kuishi kwenye jumba la fahali mishahara yao nk iko juu, watoto wao wanasomea shule za gharama , lakini likija suala la wafuasi walio wengi, HAMNA FEDHA

hizi si ni hadaa?? hivi tutakuwa lini na jamii ya wasema ukweli na sio hadaa?? sisa siasa mpaka lini?? najiuliza tu jamani

No comments: