Thursday, September 9, 2010

uchawi-HITIMISHO

labda sasa tuhitinishe mjadala huu wa kiuchawi uchawi kwani ni mrefu sana kwa hiyo tuishie pahala hapa hata hivyo katika madude ya kiuchawi uchawi kuna vitu vingi vingi kama vile kuruka kwa ungo, mapenzi ya ajabu ajabu yanayoaminika kuwa ni uchawi kwa wale waaminio hivyo

tunasikia watu wanazindika, wanatafutia kazi na kupanda vyeo, kwa kiasi kikubwa uchawi unazuia ubunifu kwani badala ya jamaa kuwa mbunifu anategemea ndumba ili kupata kazi fulani au kupanda cheo na hata kuleta migogoro, visasa na mikasa visivyoisha kazini na mambo mengineyo.

ila sasa uchawi kuwa unaleta kinga, waganga wa kienyeji hujitajirisha huku wakiipotosha jamii na mauchawi yao ambayo mengi ni mikwara au kanuni hasi. tukijiaminisha juu ya uchawi basi twaishi kama miili badala yakuishi kama SISI halisi kwani tunaamini watu fulani wanania na uwezo wa kutuloga

watu wenye roho mbaya! wanaochukua wake/ume za watu nk huchukuliwa kama wachawi kutokana na labda negative zao wazalishazo. kuna hadithi za kusafiri kwa Ungo ambazo labda hazipo au zinahitaji utafiti zaidi

ikumbukwe tu kwamba kuna nguvu nyingi za ziada alizonazo binadamu lakini nguvu zote hizi ziko chini ya uwezo wa binadamu kwani zinalazimika kufuata kanuni za maumbile na sio ajabu kujua kuwa kuna nguvu hizi kwani katika karne hii ya ishirini namoja binadamu anazidi kugundua nguvu za ziada nyingi alizonazo

angalizo ni kwamba kuna vitu ambavo kwa kweli haviwezi kujadiliwa hapa katika nguvu tulizonazo kwani vinahitaji umakini sana kwa wasomaji vinnginevyo vyaweza potosha. vitu kama uwezo wa kupaa angani, kutoka nje ya mwili wako, kupata baadhi ya vitu/mahitaji nk

wanaotaka kujua zaidi ni vyema wakawa na mwalimu wa karibu anayejua mambo haya ili wajua vyema kanuni na waweze kutumia nguvu chanya kuzalisha chanya badala ya kinyume chake

wasalaam!

3 comments:

SIMON KITURURU said...

Ingekuwa bomba kweli kama mchawi angalau mmoja angeanzisha blogu na kutoa data zaidi kutokana na uzoefu hata KI-anonymous kwa kuwa mpaka sasa naamini stori nyingi za uchawi watu tuzijuazo ni za ubunifu tu na utunzi wa ambao hata uchawi/mchawi hawajawahi kumshuhudia.:-(

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kwa jinsi nisivyopenda kuruka na ndege wallahi akitokea mchawi mmoja akafungua shule ya kufundisha watu kuruka kwa ungo mimi nitajiandikisha mara moja!

Kwa nini mambo haya yanafanywa siri sana na yanakwenda kwa mtindo wa kurithishana tu? Kama kweli tungekuwa na usafiri wa aina hii, leo hii Afrika tungekuwa wapi?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@kitururu yawezekani ni kweli. @matondo, kwa kweli swala la ungo ni gumu na labda litakutishia zaidi. kama unaogopa ndege iliyofungwa vizuri, unakaa au hata kulala, itakuwaje ungo ambao kama kweli usafiri huo upo watu wanakwenda uchi na kanunui lukuki?