Tuesday, September 7, 2010

uchawi na umasikini

kwa kiasi kikubwa labda tukubali kwamba kuna uhusiano wa karibu sana kati ya uchawi na umasikini. ukiangalia nchina tanzania mauaji ya albino, vikongwe nk utagunuda kitu

mara nyingi jamii masikini ni jamii yenye changamoto kubwa za kimaisha huku ikiwa na suruhu ndogo au haina suruhu za changamoto hizo na hivyo imani huzuka. kumbuka pia maaarifa / elimu katika jamii hizo ni ndogo na hivyo katika kila jambo watu hubakia kumtafuta mchawi

kinachofanya watu kuuwa albino au vikongwe ni ile hali ya kuchanganyikiwa kwa kukosa majibu ya maswali yanayo itatiza jamii hiyo kwa kiasi kikubwa na hivyo mawazo potofu huweza kuigia

nafasi ya imani pia ina umuhimu wake. mifumo ya imani ya jamii zetu ni kutishiana na kutiana woga usio kuwa na maana na hivyo watu kushindwa kuwa na misimao na hivyo kwendelea kutafuuta ahueni sehemu zingine

ebu angalia jamii zetu hizi za mikwara, ni lini uliwahi kwenda kwenye nyumba ya ibada usipigwe mkwar? wakati mwingine huwa tunashindwa jinsi ya kumuepuka Mungu wa dini zetu mwenye moto, viboko, hukumu na hasira kibao na hivyo kutafuta ahueni sehemu nyingine japo naku huishia kubaya zaidi kwani ni mikwara zaidi

hivyo basi uchawi una ka-uhusiano na umasikini

No comments: