Monday, October 11, 2010

changamoto ya mafundisho ya Kristo

ndugu,
katika mjadala wa dini nakutana na changamoto hizi juu ya mafundisho ya Kristo

la kwanza ni kuhusu siku ya hukumu ambayo inasemekana yaweza kuwa leo! siku hiyo ya hukumu iambatanayo na kurudi kwa yesu mwenyewe yasemekana kuwa yaweza kuwa leo tangu Kristo mwenyewe akiwa duniani mpaka sasa! huwa nawashangaa jamaa wanaoniambiaga kuwa tuko kwenye siku za mwisho, swali langu huwa ni kwa nini dunia iishe leo?

eti yaliyoandikwa yametimia! wewe uliwahi kuishi lini ambako yalikuwa bado kutimia?? kwanini mabaya ndo yamalize ulimwengu na sio mazuri?? lakini pia ni kwa nini dunia isiishe siku lukuki kabla hujazaliwa?? mtu ana kwambia dunia inaisha wakati yeye atakufa na ulimwengu utaendelea kuwepo

kubwa zaidi ni mchungaji anayekuhubiria kuwa hizi ni nyakati za mwisho na ulimwengu unaisha, harafu ukimwona mke wake ana mimba changa, sasa kama ni mwisho wa ulimwengu mchungaji anampa mimba mkewe ya nini?? si aache tu? si ni hadaa hiyo?? bora angesema padri, asiyeowa kiwazi wazi!

changamoto nyingine ni kile alichosema Yesu kuwa atarudi, lakini pia anasema kuwa yupo mpaka ukamilifu wa dahari! sasa atarudije kama yupo?

mimi ni mzazi sasa nina kazi ya kukafundisha katoto kangu vitu kama hivi ili kavielewe vyema!

No comments: