Wednesday, October 6, 2010

din; unadhani nilistahiri kupigwa kwa swali hili?

nilipokuwa kijana wa shule ya msingi nilijikuta nikipokea maonyo, makofi. viboko na mikongoto kadhaa kwa udadisi wa kiutoto na kiubinadamu wa kutaka kujua hata yaliyojificha!

basi ilitokea kijiji chetu kikavamiwa na majambazi na wadokozi kila familia lakini pia ndio wakati ambao magonjwa kama maralia ukimwi nk yalikuwa yakishika kasi. basi tulienda kanisani kukomba na ili mchungaji atuombee tuyaepuka haya majangazi

basi kanisa la kijijini kwetu lilikuwa limewekewa vioo vipya kwenye madirisha, kesho yake tulikuta vioo vile vimeibwa!

pia baada ya muda, mchungaji wetu aliugu na kukimbizwa hosp.moja ya rufaa hapa nchini. sasa swali kwa bibi yangu na kwa walimu wangu wa dini lilikuwa ni je! kwanini hii nyumba ya Mungu tunayoitumia kuomba majambazi waokoke, na yenyewe imeibwa vioo? Mungu yuko wapi na atawezaje kutulinda kama hawezi kuilinda Nyumba yake mwenyewe??

swali jingine kwa mwalimu wangu wa dini lilikuwa ni kuhusu afya ya mheshimiwa mchungaji. kwamba yeye anatuombea tusiugue, sasa inakuwaje yeye anaugua na kukimbizwa hospitalini? kama hawezi kujiombea atatuombeaji sis wazima?

wewe!! kilichotokea mwalimu wangu wa dini alinifokea na kuja kunishitaki kwa bibi, bibi yangu akachanganya na kosa la swali la kwanza!! nilitukanwa kila aina ya tusi na kupigwa viboko na makofi, nilambiwa kuwa ni kufuru na hivyo niliadhibiwa ili nijirudi nisije enenda kwa shetani

wewe unadhani nilistahiri kipigo kile kweli??

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Staili ya kufunza watoto Tanzania ni ya vitisho kweli na makonzi juu. Ukiwamdadisi lazima ubwengwe makonzi na kufinywa sana tu ndio maana mara nyingine ukifananisha watoto wa Tanzania na kwa mfano wa Ulaya magharibi wenye lika moja unaweza kudhani Wamagharibi wanaakili zaidi kumbe walichonacho ni uhuru wa kusema maoni yao kwa wakubwa huku wakisikilizwa ndicho kiwafanyacho wawe huru kutamka wanachojua.

Sasa unakuta mtoto ukidadisi kitu ni kutukanwa mjinga au tu kudhaniwa Mkorofi mwishowe unakuwa mtu mzima ambaye hajiamini. Halafu watu wanashangaa ukienda hata kudai maslahi yako kwa wakoloni kazi ni kujichekesha halafu YES YES kwa wingi wakati rohoni unabonge la NOO ila unashindwa kulisema kwa kutojiamini ulikojengewa tokea utoto.:-(


Kipengele ambacho nilikipata katika redio za mbao:

Ila nasikia MAO huko Uchina wakati anafuta dini alikuwa anatumia gia hizo za kuonyesha kuwa kama kuna MUNGU mbona mkijificha kanisani kanisa likipigwa bomu mnakufilia mbali na Kanisa linafutika?

... sina uhakika labda ni LENIN huko Russia ndio alikuwa anafanya hivyo.:-(

emu-three said...

Tatizo la dini wengine walitaka watu wapokee kama yalivyo na kusiwe na udadisi.
Kwasababu gani, hata wao hawana maibu rahisi. Hii imewafanya watafiti wachakachue ukweli na walipogundua wakaona wanadanganywa na kutafuta ukweli ulipo na matokeo yake `ni kuhama' kwanini nifichwe ukweli!
Mtu anafanya makosa anakwenda kutubu makosa kwa mtu ambaye anafanya makosa zaidi yake? Kwanini usitubu mwenyewe kwa muumba wako? Hili ni swali ambalo nilikuwa nikijiuliza na nilipoulizwa niliishiwa kutaka kuchapwa kama wewe...