Friday, October 15, 2010

Dr. Slaa Bukoba sijawahi ona mimie

Nikiwa najielekeza kwenye viwanja vya mashujaa ili kusikiliza sera za mgombea kama ilivyo kawaida yangu kwa wagombea mbali mbali, nakutana na foleni za magari, magari hayaendi na ni foleni mithili ya dar! Nashangaa Bukoba na foleni, mara misururu ya watu

Wanamsubilia mgombea urais kupitia chadema! Du ni hatari, wingi wa watu ,mara misafara ya piki piki, mara baisikeli, helkopta kwa juu aisee ni kali hii, Dr. slaa huyo ndani ya Toyota Hilux, watu wanakimbizana, wanajaza bara bara, hata polisi waliovalia maguo ya kutisha hawauwezi umati huu

Ni hatari, watu wanakimbilia viwanja vya mashujaa, sijawahi ona mimi umati huu. Slaa anapanda jukwaani mara moja! Anahutubia kwa muda wa kama saa moja hivi, hasomi popote, watu wanashangilia, wanavumilia kusimama jua kali na joto kali

Hamasa ni ya hali ya juu mjini hapa. Ili kupata sera za huyu bwana, ni lazima kuhudhuria kampeni zake, maana baadhi ya “madongo” yake hamna mtu anaweza kuyarusha kwenye vyombo vyetu vya habari kwa kweli hali ni ya ajabu hapa

Sijui nini kinatokea mwaka huu na Chadema!

3 comments:

Subi said...

Afadhali ulifungua blogu Kamala na kwamba unaiendeleza kwa kupasha ulimwangu habari. Hii ni mojawapo ya kumbukumbu katika masuala ya Uchaguzi Tanzania 2010.
Asante sana kwa simulizi la hali halisi kwa jinsi ulivyoiona wewe.
Iko haja ya kuchukua tathmini zote, zikalinganishwa na miaka iliyopita na miaka ijayo, wenye kutafiti mwelekeo wakagundua wapi makosa yanatendeka na wapi pa kurekebisha (kwa vyama vyote, chenye hatamu ya uongozi na visivyokuwa navyo, wanalo la kujifunza, ikiwa wana nia).

Shukrani sana Kamala!

John Mwaipopo said...

nagandamizia "Anahutubia kwa muda wa kama saa moja hivi, hasomi popote, watu wanashangilia, wanavumilia kusimama jua kali na joto kali"

HASOMI POPOTE

ndiye huyu masihi tuliyekuwa tukimsubiria

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

asante Subi kwa elimu hii

@mwaipopo naona kama uko sahihi vile!