Tuesday, October 12, 2010

maombi / sara za kulazimishwa!

nimelelewa kwenye familia ambayo mbele za watu ilitaka ionekana au iaminike kuwa ni familia ya kikristo a.k.a ya kilokole na kwa hiyo usiku baada ya msosi ilibidi tukae, tuimbe na kusali! tunaimba kwa sauti mpaka majirani nao wasikie

basi bwana, kukaa pale kwenye sara ilkuwa lazima. ishu ni msalishaji kusema maneno lukuki, mwisho wa sara asilimia hamsini iliisha sinzia ile mbaya!! tuliamshwa kwa mikwara tukalale

ngoma ilikuwa nzito usiku mwingine ambapa sara a.k.a maombi zilifanyika kabla ya msosi wakati msosi wenyewe uko mbele yenu! acha jamaa linasali sara ndeefu wakati wewe unanjaa, linasali wewe unatukana kimoyomoyo!!

imani zetu jamani

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala; Hiyo imani ni nzuri sana binafsi tulikuwa tunasali kabla ya kula chakula, baada ya chakula. Kabla ya kwenda kulala na asubuhi tukiamka. Na kama ulivyosema ni imani zetu. Lakini mimi nilikuwa napenda kwa sababu ndo hapo mtu ulikuwa unajifunza. Ni kama vile WIMBO wa TAIFA sisi waTanzania tunaimba kabla ya kuingia darasani na kabla hatuaenda nyumbani kwa mtindo huu nadhani hakuna mTanzania asiyejua kuimba wimbo wa Taifa. Kwani kuna nchi nyingine hawawezi kabisa wala hata kusali sala ya baba yetu.

SIMON KITURURU said...

Kusali kabla ya kwenda kulala kumbe wengi tumepitia. Tatizo la kulazimishana kusali unawatia bure watu dhambi zaidi. Ona sasa katika mfano wa Komandoo Kamala: wewe unakazana kusali mwingine anazinguka na kutukania kichinichini kisa anasubiri umalize msosi uliwe- au analala na akiamka sala zimekwisha unakuwa ushamtia majaribuni .


@Yasinta:
Kuna pati fulani ya Kitanzania niliipitia na hakuna aliyekuwa anakumbuka maneno ya nyimbo hizo tokea mwanzo mpaka mwisho bila kuboronga na pati yenyewe ilikuwa mitaa ya Scandinavia ambako upo. Kwa hiyo kusema kila Mtanzania anajua wimbo wa Taifa hata pia nyimbo nyingine za Kitaifa labda sio kweli kwa wote.

Ingawa inaweza kuwa WATU wanajua kama wanaimba na watu wengine kwa kudakiadakia wakikumbushwa maneno kwa kusikiliza watu wengine.


Nyongeza:
Hata mimi kutokana na kukariri nyimbo na sala za Kikatoliki na Kilutheri , mara kibao hudhania nimezisahau ila nikisikia tu mtu mwingine anasali au kuimba zinanijia mukichwa ila ukiniacha mwenyewe Sala ya Maria + nyimbo bwelele hazipandi tena.

John Mwaipopo said...

ni 'sala' sio 'sara'. tunasali, hatusari

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

AMEN