Thursday, October 21, 2010

mgombea hawashangaa wananchi wa BKB kukimbilia helkopta ya Slaa

kama vile haitoshi mgombea mmoja katika kampeni yake ametumia muda mwingi kumshambulia dr Slaa wa chadema kwa maneno ya ajabu na sio sera

kubwa zaidi mgombea huyo aliwageuzia kibao wananchi aliokuwa akiwahutubia kuwa ni washamba wa kuikimbilia helkopta ya dr. Slaa

alisema "yaani wananchi wa mkoa huu mnashangaza, mnakimbilia kushangaa helkopta"


japo hakuonekana kujibu hoja na sera zinazochoma moyo za Dr Slaa, aliwashangaa washamba anaowaomba kura kwa kukimbilia Helkopta labda badala ya shangingi

8 comments:

Subi said...

tehe! ha ha ha. Badala ya kutangaza sera, akaanza kusemea wananchi mbof mbof nha ha ha ha. Siasa zinaendelea kukua, inavutia kuona changamoto hizi.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Huyu mgombea naye bomu tu. Mbona asingepita njia ya mkato na kuahidi kuwanunulia helikopita kila kata kama wakimchagua?

Kwa siasa za Tanzania unaweza kuahidi cho chote unachotaka bila wasiwasi wa kuja kushikwa shati baadaye kama ilivyo kawaida kwa nchi za wenzetu hizi.

Hebu uchaguzi uishe tupumzike!

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Sasa nakwenda nje ya mada kidogo.

Kule kwa Subi nilijaribu kuzusha hoja mbadala nikakataliwa:

http://www.wavuti.com/4/post/2010/10/beh-tuache-kukichinja-kiswahili-hivi-kikifa-je.html#axzz130bjJk42

Sasa ushahidi huu hapa laivu kabisa (Kamala usikiguse kichwa cha post hii kwani naamini siyo typo).

SIMON KITURURU said...

Naunga mkono na miguu hoja hii ya Mkuu Masangu Matondo:

``Hebu uchaguzi uishe tupumzike!´´

John Mwaipopo said...

no! mie nataka uchaguzi uendelee maana uchaguzi unaporefushwa wale vijana wa bongofleva wanaoambatana na chama fulani wananeemeka zaidi. bongofleva wananyonywa sana na wadosi a.k.a wahindi. ngoja usogezwe mbele bongofleva wanunue magari na wajenge nyumba.

John Mwaipopo said...

no! mie nataka uchaguzi uendelee maana uchaguzi unaporefushwa wale vijana wa bongofleva wanaoambatana na chama fulani wananeemeka zaidi. bongofleva wananyonywa sana na wadosi a.k.a wahindi. ngoja usogezwe mbele bongofleva wanunue magari na wajenge nyumba.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Mwaipopoooooo!

Dah! Leo umemshika pabaya Kamala@MMN

Subi said...

Prof Masangu, sasa hivi damu za Watanzania zimelewa uchaguzi, hizi hoja na habari nyingine ni nadra sana kumkuta mtu anazisoma mara mbili, tusubiri tu kama ulivyosema "uchaguzi uishe tupumzike!" itatusaidia kupumzika habari za siasa na uchaguzi walao tutaanza kujadili 'yatokanayo' na kuanza kurusha madongo upya kwa atakayeshika hatamu ya uongozi. Hapo ndipo tutaweza kurejea kwenye kujadili mada za 'kiswahili kuchinjwa' na umuhimu wa 'kufahamu nia na kusudi la msemaji au mwandishi' na lengo lake kwa hadhira yake kwa wakati huos.