Friday, October 22, 2010

napigiwa simu juu ya kura kwa Slaa

ndugu jamaa na marafiki na nani sijui wananipigia simu lukuk wakitaka kunijulisha kuwa wao watampigia kura Dr. Slaa!

nashangaa kwa nini wanipigie simu hizi, je nia yao ni kunishawishi nami nimpigie au ni kuwasilisha hisia zao kali juu ya huyu jamaa

wewe unaonaje

4 comments:

emu-three said...

Zote ni mbinu za kisasa, mwisho wa siku ni wewe na kura yako, wengine wanasema kura zimeshapigwa!
Sijui hilo `wao wasema' kama mcha mungu mungu wa kweli ukiwa ndani ya chumba chako cha kupigia kura utajiwajibisha mwenyewe, kwani mwisho wa siku kura yako hiyo itakuuliza kwanini ulinitendea hivi, badala ya kunipigia kwa wema umenipigia kwa wabaya na nimehusika kuwaangamiza wasio na hatia, nimehusika kuwalaza watoto wa walalahoi njaa, nimehusika kuwanyima haki wenye haki...kwa vile umemchagua fisadi ukijua kweli ni fisadi...kura hiyo jama, angalieni itawatia motoni, mkiifanya vibaya!

Subi said...

Hilo lako, unalo! Mi langu ni hili, "Ole wako usipige kura" nitakucharaza viboko tu! Tafadhali tafadhali Kamala, sijali unayempigia kura, ila nakuomba chonde chonde usiache kupiga kura na usiache kuwashawishi wengine kupiga kura. Hii itakupa nguvu ya mahali pa kusimamia utakapoanza kuchambua yatokanayo na uchaguzi huu (ikiwa utataka). Piga kura Kamala!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@subi, naamini nitakuwa wa kwanza kituoni kupiga kura, halina ubishi

Subi said...

Asante sana Kamala kwa ahadi, na nina amini utaitelekeza bila tashwishi! Nimefarijika! Go Tanzania Go!