Tuesday, October 26, 2010

natisha


mtaani kwetu naogopwa. naishe kwenye staff kwotas na kwa hiyo ni sehemu ambayo watu twajuana, sio uswazi kama zilivyo swazi nyingine. sasa basi, mtaa ule naogopwa kinoma, eti natisha, sura yangu kali ni serious na nini sijui


hata walinzi wa mtaa huu wananiogopa, nashangaa kuogopwa na watu wenye bunduki wakati mimi sina hata kisu, eti natisha, si mnajua mazoezi kidogo?


wakati mimi ni mtu wa kawaida saana, najitahidi kuishi kwa upendo, kwa amani na kuwathamini wengine. naogopa hata kula kiumbe kilichouwawa kwa upendo, sasa iweje watu waniogope hivyo?


wanaagalia nje na sio ndani. naishi na binti mmoja pale nyumbani kwangu, vijana wa mtaani hawasogei pale, wanaogopa figure.


ila sasa ngoma nzito kwa ninaoongea nao, natumia nguvu ya hoja na hivyo ni lazima kujipanga kabla hujaongea. duh kiumbe gani mimi


siku moja niliteuliwa kuwa refa wa mchezo mmoja hapa mtaani kwetu, wewe! kama wafokewavyo marefa, ilikuwa nidhamu na lawama zilitolewa mbali sana nisije jua fulani kasema hivi


jamani mimi ni mtu simple, social, mtu wa Mungu nk, sitishi kama idhaniwavyo

8 comments:

Subi said...

Nimekusoma. Nimekuelewa.
Kamala, mtu asipochukua muda kukukufahamu, ni rahisi sana kuondoka na taswira potofu. Awali nikisoma maoni yako, nilikuwa nashindwa kabisa kuamini kuwa unalo neno hata moja la upendo, lakini nilipoendelea kukusoma na kubadili fikira zangu kuhusu wewe, nimegundua kuwa wewe ni mmojawapo wa watu wanaopenda sana changamoto na kutizama jambo kwa upande wa pili, lau liwe chanya ama hasi, yaani kwamba, ijapokuwa unaufahamu mwelekeo mmoja wa walio wengi, huwa unapenda kuwaza na kuonesha mwonekano wa pili ambao wengi aidha hawaufahamu au kutokana na kuufahamu kuwa haupendezi masikioni mwa wasikilizaji au machoni pa watizamaji, huwa 'wanauchunia'. Nimefurahi kusoma maelezo ya wasifu wako mwenyewe toka kwako mwenyewe! U mtu mwema!

Mija Shija Sayi said...

Wakati mwingine ni afadhali kuogopwa kuliko kutoogopwa...

Bless you kaka.

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana na dada zangu waliotangulia hata mimi mwenyewe kabla sijakufahamu kwa kusoma maoni uliokuwa unatoa nilikuwa najiuliza huyu binadamu ana maanisha nini na yupoja kiupendo na mawazo. Ila sasa nina amani kabisa na Kamala kwa hioyo hao wanaokuogopa wanakosa mengi.

emu-three said...

Mhhh, zimwi likujualo halikuli likafanya nini vile!!!?

John Mwaipopo said...

mie sihawahi kuwa karibu na wewe na nakuogopa je walio karibu!

tehe!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@da subi kumbe inahitaji muda, hata wanafamilia nao unigwaya

chib said...

Kamala mimi nimemuweka kwenye controversial group. Kwangu watu wa namna hii ni muhimu, kwani huwa wanaipa maarifa ya kuangalia ule upande ambao siuangalii mara kwa mara. Nikiona ujumbe wake, naanza kucheka, maana wakati mwingine unaweza kujikunjia ngumi peke yako bure yako.... :-)

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Da Subi - hata mimi umenisemea na sina cha kuongezea.