Wednesday, October 27, 2010

pole kwa bwana kaijage

natoa pole zangu za dhati kwa ndugu yangu wa hiari mwanasheria Danstan kaijage wa huko changanyikeni Dar es salaam kwa kondokewa ghafra na mdogo wetu wa kike ambaye alikuwa na siku mbili tu tangu amalize kidato cha nne

msichana Anna alikufa usingizini usiku wa kuamkia jumanne na inasemekana labda ni ugonjwa wa moyo

natoa salamu za rambi rambi kwa ndugu yangu Danstan na familia yake yote na naowaombea wote kuwa na uvumilivu na imani ili matokea yaliyopangwa na NGUVU ipitayo uelewa wetu yapokelewe na kukubaliwa

AMINA

4 comments:

chib said...

Poleni kwa msiba

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Habari mbaya hizi. Mungu Amrehemu!

Albert Paul said...

Poleni sana wanafamilia, wanandugu, jamaa na marafiki, ni kipindi kigumu kwa hakika, Mungu awape nguvu na ujasiri.
Mungu alitoa, Mungu ametwaa, jina lake lihimidiwe.

emu-three said...

Poleni sana kwa msiba yote mapenzi ya muumba!