Wednesday, October 20, 2010

tuangaliea sara hii ya kibiblia

matayo 20: 20-23

20.
Hapo mama yao wana wa Zebedayo alimjia Yesu pamoja na wanawe, akapiga magoti mbele yake na kumwomba kitu.
Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.

21. Yesu akamwuliza, "Unataka nini?" Huyo mama akamwambia, "Ahidi kwamba katika Ufalme wako, hawa wanangu wawili watakaa mmoja upande wako wakulia na mwingine upande wako wa kushoto."
Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.

22. Yesu akajibu, "Hamjui mnaomba nini. Je, mnaweza kunywa kikombe nitakachokunywa mimi?" Wakamjibu, "Tunaweza."
Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza.

23. Yesu akawaambia, "Kweli mtakunywa kikombe changu, lakini kuketi kulia au kushoto kwangu si kazi yangu kupanga; jambo hilo watapewawale waliowekewa tayari na Baba yangu."
Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu


je unaelewa nini hapa?? ndio tatizo la sara na maombi yetu, tunaomba tusichokijua. ila sasa hawa jamaa aliona Yesu ni maarufu, anapendwa na watu nao wakatamani u-supestar kwa kuwa karibu naye, nafikiri walipoona anauwawa na kufinnyangwa walifurahia na kujipongeza kwa maombi yao kukataliwa

No comments: