Monday, October 18, 2010

tunaamini / kuabuni Miungu!

katika mada juu ya dini kuna ka-ukweli kanako uma japo kidogo. ukiangalia utitiri wa dini na madhehebu utaamini kuwa tunaabudu vijimiungu vyetu.

kwamba kuna Mungu wa kiisilamu atakaye yale wafanyayo waisilamu na kuna Mungu wa kikristo afanyaye yale ya wakristo.

lakini pia ndani ya ukristo kana Mungu au Kristo wa dhehebu falani afanyaye yale yasiyofanywa na madhehebu mengine na kuna Mungu wa dhehebu jingine!

maandishi matakatifu ni magumu sana kuyaelewa na ndiyo maana tofauti kati ya pentekoste na katoliki /uluteri ni ubatizo! wapentekoste wanataka jamaa azame mzima mzima mtoni bila kujali samaki watamchungulia nyeti zake lakini kuna mamba au kiboko, atajisevia mwili ule!

tofauti kubwa kati ya uluteri na ukatoliki ni kuinjoy nyeti za viongozi wa dini kwamba wakatoliki wasioe hadharani au hata sirini lakini waluteri waoe wazi wazi. Hili halijasaidia chochote katika dini zetu kwani bado wote hufumaniwa!

kila dini ina kaji-Mungu kake na hivyo Miungu ni mingi!

unabisha??

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kaazi kwelikweli hapa:-)

Subi said...

Sibishi Kamala naunga mkono na mguu (japo sina gundi ya kuungia).
Uliyosema ni sawa, kila dini/dhehebu hujiona bora zaidi.
Mimi nadhani dhehebu ni utaratibu ambao kikundi cha watu wamekubaliana na kuafiki kuwa kwa imani yao na tafsiri ya kitabu wanachokiamini, hivyo wafanyavyo ndiyo njia sahihi zaidi ya kumwabudu Mungu kuliko wengine. Wengine huzaliwa wakakulia na kufia dhehebu hilo, na wengine huhama na kujiunga na wale wanaoafikiana nao.

Tafsiri ya dini nadhani itajumuisha tafsiri ya dhehebu na kuongeza kuwa ni imani anayoirithi mtu kutoka kwa wazazi au walezi wake au kujiunga baada ya kusoma vitabu vya dini hiyo.

Ila ni kwa nini dini zote huonekana (walao kwa kusoma vitabu vyao) kuhubiri upendo, amani na umoja wa kibinadamu il hali inavyoonekana katika maisha ya mwanadamu (walao kwa kufuatilia taarifa za habari), utengano na machafuko mengi yametokana na tofauti za kidini? Hapo ndipo dhana nzima ya dini inaponipiga chenga.