Friday, October 8, 2010

Uislamu, ndevu na ugaidi


tukijadili masuala ya dini kuna changamoto nakutana nazo mimie!! napenda sana kufuga ndevu kama nitakavyoonyesha picha yangu siku zijazo iliyojaa ndevu, ila sasa nalazimika kuzinyoa kutokana na ukweli kuwa mimi ni mutu ya kusafiri sana katika ulimwengu wa waisilamu, wasio waisilamu (wakiwemo wakristo) ni makafiri fulani hivi, lakini hata ulimwengu wa wakristo nao waisilamu ni magaidi.

vile vikosi vya kigaidi kama vile taliban, binladen, alkaida, alshabaabu nk hufananishwa na uisilamu, ugumu ni kudhibitisha kama kweli vikosi hivi vipo au ni propaganda za watu fulani dhidi ya dini fulani
ila sasa, vikosi nilivyovitaja hapo juu hufuga ndevu na waisilamu wengi pia hufuga ndevu,

mimi binafsi najikuta nikipenda saana kufuga kidevu, kukiacha kiwe kireeefu, cheusi kama nini sijui. ila sasa katika ulimwengu huu ambao ufugaji ndevu hufananishwa na uisilamu na ambapo waisilamu wengi hufananishwa na ugaidi, najikuta nikiwa mwoga wa kufuga ndevu
nina wasi wasi kwamba kuna baadhi ya maeneo mtu ukiwa mweusi na ukawa na ndevu ndefu basi unaweza kujikuta mikononi mwa sheria kali za kiuonevu na kufananishwa na ugaidi na kwa hiyo nalazimika kunyoa ndevu hiizi na kubakiza kidogo tu

naonewa na misingi ya dini zenye mambo mengi hapa duniani
ni dini zetu jamani

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala basi usinyoe kwanza tuonyeshe ni vipi unaonekana na ndevu na halafu bila ndevu. Lakini hizi zote ni imani tu.

Anonymous said...

Madefu marefu ni mila za wajukuu wa Ibrahimu wote (Waisraeli na Waarabu)!

SIMON KITURURU said...

Mmmmmh!