Wednesday, November 24, 2010

dini / maisha yetu eti hadi Mungu atahukumu vibaya!najikuta na swali juu ya dini zetu kila nijongeapo karibu na Nyumba za Ibada. napenda sana kwenda kanisani kwa sababu nyingi tu za Msingi lakini kila niendapo huko huwa nakuwa na maswali nisiyioweza kumuuliza yeyote kwani hakuna jibu!

sasa inahubiriwa juu ya hukumu, eti siku ya mwinsho mungu na yesu watakuja na hukumu ya kukata na shoka! eti watenda dhambi a.k.a kuonyesha uhalisia wao hadharani kama vile kupenda ngono, ulevi, umbeya nk watahukumuiwa vibaya na kutupwa Motoni!
binadamu tumekuwa watu wa Kuhukumu wenzetu!

tunahukumu, hatuchukuliani wala kubebeana wala kupendana wala kufikiriana! utasikia jamaa anakuhukumu eti wewe ni fala, wewe jinga, malaya, mbwa nk! yaani unahukumiwa direct bila hata ushahidi wala utetezi wa wakili!
sasa ndo tabia hii ya kuhukumu wenzetu tunamhusisha na yule bigbro tumwitaye Mungu a.k.a sir God! eti atakuja kuyahukumu vibaya matenda dhambi!

kauli hizi utolewa na walokole zaidi! ila hakuna hata mmoja wao ajiwekaye katika hukumu hiyo ya kwenda motoni ila huwaona wengine wakienda motoni!
Mungu hatahukumu bali wewe ndo unajaribu kumwambukiza tabia ya kuhukumu na kwa taarifa Yako Mungu ana kinga kali na kamwe hautomwambikiza hadanganyikiiiiii

sasa wanadai eti na Yethu naye atarudi kuhukumu! wewe!! mbona hakuhukumu hata kidogo alipokuwako hapa kwetu a.k.a mavumbini?? ni wapi yethu alihukumu?? nionyeshine jamani! ila yeye alidai kuwa hakuna kuhukumu wala kuharibu, ila alikuja kwa ajili ya wakosefu na waliopotea na ndio maana alishinda vijiweni akiwahubilia malaya, vyangudoa, mateja, walevi na wavuvi sasa iweje tumwandalie hukumu wakati sio urith wake??

we endelea kuhukumu ukijidanganya eti utamwambukiza MUNGU, utakuta umejihukumu mwenyewe, acha ujinga

1 comment:

emu-three said...

Mara nyingi twapenda kunyosheana vidole, ni rahisi sana, hebu jaribu kumnyoshea mwenzako kidole, na uone hekima ya maumbile aliyotupa mungu.
Ukimnyoshea mwenzako kidole,, kama una vidole vyote sawa angalia ni vingapi vinakuonyoshea wewe! Ni kuwa kama mwenzako katenda dhambi moja, wewe huenda umetenda zaidi ya matatu...hujioni, waona ya mwenzako! HEKIMA ILIYOJE NDANI YA MAUNGO YETU WENYEWE!