Tuesday, November 16, 2010

dini zetu na kuzika wafu kidini / kikristo!


siku kadhaa zilizopita nilihudhuria mazishi ya bibi wa rafiki yangu ambaye anasomea upadre na yuko hatua za mwisho za kuwa padre a.k.a mtoa dogma au laana usipofanya yale atarajiayo kukushurutisha kuyafanya

lawaida yangu nihudhuriapo mazishi yoyote huwa naangalia kama sinema na kujifunza mengi kutokana na mazishi yenyewe.

na hivi karibuni nimehudhuria mazishi ya mama wa rafiki yangu mmoja. nimeona mengi, wahubiri wa mazishi yale au mapadre huwa wanafokea wazikaji waliobaki kuwa hawaendi kanisani na hivyo wakifa hawatazikwa au wakifiwa!

huwa najiuliza maneno na ibada tuzifanyazo huwa zinamhusu nini yule aliyekufa kama sio kujipa moyo sisi tuliobaki na kujiaminisha kuwa marehemu kaelekea kwenye pilau za bure na nyama badala ya kulazwa kwenye nge na funza

ila sasa, hivi karibuni kuna jamaa kafiwa na padre asije kuzika, kilichotokea pale msibani, kajiteua jamaa mmoja akiwa ameonja kilevi na kuongoza ibada na kuzika vyema! niliiipenda hiyo kwani hakukuwa na kesi wala kumbembelezana wala kukusanya pesa a.k.a sadaka kwa ajili ya padre na nani sijui

maendeleo ya imani hayo

2 comments:

chib said...

Sasa huyo jamaa pombe ndio ilimtuma na kujifanya ni kasisi :-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hapo sasa