Monday, November 8, 2010

duhu, miaka Minne sasa bloguni wandugu

November ni mwaka mwingine wa blogu hii a.k.a Kijiwe chetu pendwa kuwa hewani. kijiwe hiki kilianza mwaka 2006, na sasa kimechumpa na kufikisha umri wa mtoto kwenda vidudu / chekechea

ilianza kama harakati za vijana, ikawa utambuzi, vituko, viburudisho elimu na majiulizo
sasa imenijengea urafiki, imekuwa shule ya kujifuza na kujifuzia, ni kiunganishi, urafiki changamoto na hata kisemeo

kwa kifupi hamna ajenda maalumu bali kuelimisha, kuburudisha, kufikiri na kufikirisha, kupatia pumziko, ahueni na hata kufikisha Jumbe

bado kinaitwa kijiwe usije shangaa kikibadilika na kuwa altare/madhabahu, hubirio, kanisa, baraza, bunge, au hata msikiti.

ila sasa uwepo wako wewe ndio mafanikio ya kuendelea kuwa hewani na ni uwepo huo unaonipa tumaini la kuendelea kuwepo

ujinga wazaa busara na busara za zaa ujinga kwa tafsiri ya atafsriye kisomwacho

ni ulimwengu wa kijiuliza, na kushangaa, free thinking, free writing, free readind yaaani hamna mipaka wala mipanya ya kujimwaga, hamna matusi bali tafsiri

nikijiwe chetu, miaka minne, happbirthiday but thanks for you being there fore me, I will be here as well

mwendesha kijiwe

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kwa kutimiza miaka minne blog ya kijiwe, nygerage, .....jina ndefu mno jamani..lol

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Hongera sana. Wengine hata miaka miwili hatujafikisha na tayari tunajikongoja.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

hongera mkubwa wa kazi! Manake nadhani hata mwaka wengine hatutofikishaga...yeeeeh!

SIMON KITURURU said...

Hongera sana Mkuu!

Baraka Mfunguo said...

HONGERA SANA KAMANDA