Saturday, November 13, 2010

Jamii yetu, ubinadamu wetu na mali za duni (fedha?)


ukiona marafiki wa zamani hawaelewani na mmoja anakwambia hataki kuonana na mwingine tena basi ujue kuna dhuluma, kutokuelewana au wizi wa mchana kweupe japo kuna kesi ndogo za kuchukuliana wake nk. i

la sasa pesa inaharibu hata ukaribu wa Mungu au dini. ukiangalia vizuri hapa nchini pesa imetawala dini zote na viongozi wa dini. huduma za kiroho nk zote sasa inalipiwa kama kodi vile. mafundisho ni kinyume na maagizo ya waazilishi wa dini
nina rafiki yangu mmoja aliyenidhulumu laki mbili nikiwa mwanafunzi na urafiki ukafa.
nikutanapo naye mtaani sipendi kumdai wala nini na hivyo hubakia kusalimiana salamu inakuwa kama ina mpaka vile
sasa inashangaza mtu hajali upamoja, utu, undugu nk. likija swala la pesa duh lugha zinakuwa nyingine.

mbaya zaidi hii ni kwa viongozi wa dini pia! hapo ndipo kazi huwa kubwa.
sasa ngoma ni nzito pale ugunduapo ya kuwa pesa yenyewe inayoleta ugomvi ni hela kiduchu tu! hapo unaushangaa hata uwezo wa akili alionao mhusika

ushauri wangu ni kwamba, pesa always huwa ndogo kwani hamna pesa iliyowahi kutosha lakini pesa pia huwa kubwa kwani kama inaweza kumaliza hitaji lako ni kubwa kwako, lakini pamoja na hayo, tuangalie pesa isiharibu utu wetu, umoja wetu, undugu wetu na hata imani zetu eti kisa, vijisenti tu

3 comments:

emu-three said...

Ujumbe murua mkuu, wa internet cafe umeisha ningeongea mengi, wikiendi njema

Anonymous said...

kweli kamara mimi nina ndugu yangu mmoja mpaka uhusiano niwamashaka sana sasahivi kwassh.15000tu.mimi nilisha msamehe lakini kinachoniuma wakati anazitaka hizo hela nilikuwa sina mkononi nikaenda kwa rafiki yangu nikajikopesha ili nimpe maana alisema kama huna basi kajikopeshe hata kwa rafiki yako nikikupa utamrejeshea rafikio sasa nlivyo mkumbushatu.matusi niliyoambulia mimi naringa na vijihela hata yeye anazo haaa????????!!!!!!!!!!

Anonymous said...

ila kamara uwe unaandika herufi unazimalizia