Friday, November 26, 2010

kukojoa mitaani / shambani, bomba kweli uhayani

ndugu zangu kana tamaduni kuna mazingira na mazoea na nini sijui.

sasa kuna watu wanaokemea wakojoa barabarani sijui wanakemea kwa misingi ya tamaduni zipi! nikiri kwamba mimi ni mmoja wa wakojoaji shambani! hivi kuna tatizo gani kama mtu unatembea mwendo mrefu porini na usiweze kujinafasiga vyema?

wabongo hupenga na kutema kokote bila kujali! hii ya kupenga na kutema mimi hunipa ka shida kadogo

lakini kuna wnaolala na beseni au karai ndani na kuweka lokojo usiku kucha then asubuhi kuna zamu za kulitapisha besini / karai hilo la koja la familia! nikiwa mdogo kijijini kwetu biashara hii ilifanyika sana sana na kila niendaapo kwetu bado inafanyia, sasa iweje barabarani

niwapo kijijini kwetu au hata shambani kwetu siwezi kamwe kumwaga kojo chooni kwani kutokana na ugonjwa wa Myauko wa migomba na wadudu wengine inasemekana mkoja ni tiba na kwa hiyo sharti ukojoe kwenye shina moja wapo la mgomba ili kuutibia!

tusisahau pia kuwa mkojo ni mbolea! kwa hiyo mnaochanganya tamaduni za wasio na migomba, sisi wakulima wa ndizi ni lazima tu tumwage kojo pale lifaapo! hata kama sio kwetu, ukishikwa na kojo basi unaenda kwenye shamba la jirani na kumsaidia kuondoa gonjwa hilo

hivyo basi, ukija bukoba usishangae kuona nakuhamasisha tukakojoe kwanye shamba moja waapo na ntakuona sio mwema ukipeleka mkojo wako chooni wakati unahitajika migombani!

jamani tusiiige tamaduni POTOFU za kutupotezea rasilimali zetu!

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hakika itabidi nije huko, kukojoa migombani ha ha ha haaaaaa:-)

Koero Mkundi said...

Kamala ingekuwa busara kama ungetumia neno "Kutabawali" badala ya hilo neno Kukojoa...... hukujifunza tafsida kaka yangu?
Ni wazo tu

Albert Paul said...

Koero, badala ya kusema 'nakwenda haja ndogo' naweza kusema nakwenda "kutabawali" ?


Kamala, mbali na sababu ulizozitoa ambazo kitamaduni ni sahihi huko Bukoba, ila kukojoa nje (huko migombani) huoni kuwa ni uchafuzi wa mazingira?, harufu kali ya mkojo inachafua hewa na kuleta bugdha.

Mimi naishauri jamii ya huko itumie tafsida kwa kutabawali (nashukuru Koero kwa msamiati) chooni.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Kukojoa plse, na sio kupiga bao!!!!

wewe albert nimekupa sababu, kwetu mkojo sio uchafu, ni dawa! utamaduni huo