Friday, November 5, 2010

MMMH, siasa ni uwongo wenye ukweli ndani ndani yake . jadili.
Hili ni swali la siasa nalikumbuka sana wakati nipo sekondari. Nililiona kama swali la utata kipindi hicho kwani `uwongo' na `ukweli' uweze kukaa zizi moja.
Sasa nalikumbuka sana hilo swali kwani nipo kwenye `vitendo' vyake, nawaona wanasiasa wanavyomwaga sera, ukizisikiliza utasema mmmh hizi ndizo sera!
Sasa wape madaraka, utakumbuka ule usemi wao, ambao mmmh, uliuona ukweli , sasa mmmh, umegeuka uwongo!

3 comments:

emu-three said...

duuh, siasa, uwongo, ukweli!

chib said...

Mimi nakumbuka wakati tunaanza kujifunza siasa darasa la 3, kuna mwanafunzi mmoja aliulizwa darasani aeleze maana ya siasa, akajibu ni uongo uliokomaa na kuzoeleka katika jamii ya watu kiasi kwamba ukaona ni ukweli uliokubuhu.
Nikaamini ndio jibu, kwani nilikuwa hata sijui siasa ni nini. Kilichonikatisha tamaa, ni kwamba jamaa alinyeshewa mvua ya bakora...., nikaichukia siasa kabla hata sijaifahamu.
Baadaye ilifahamika kuwa mtoto huyo alikuwa akimsikia mjomba wake akisema kuhusu siasa, naye akamnukuu, kwa hiyo naye alikuwa anajua hiyo ndio maana ya siasa.

Candy1 said...

Tumeshawazoea! Tutafanyaje? Hamna wala afadhali nchi wala sehemu yoyote ile, mambo yale yale! anyway!