Thursday, November 4, 2010

politics, siasa, si-hasa

tuachane na uchakachuaji wa ajabu, inashangaza vyombo vinavyoaminikakuwa ni vya usalama japokuwa vyenewe si salama kwani vinabeba siraha hatari na hivyo penye hatari si salama! vinavyowatwanga wananchi wanaosubilia matokeo ya kura walizopiga wenyewe!

ila sasa hapa kunamambo ya ajabuz pia. lakini labda ndio siasa, kiongozi achaguliwaye eti anapendwa hutumia pesa kibao kununua siraha kama vile maji ya washa, mabomu ya machozi nk, kiongozi huyo inadaiwa kuwa anapendwa japo anawalinzi wa kumlinda dhidi ya wampendao

mtaalamu wa meditation na masuala ya kiroho Osho anasema hivi; siasa za vyama vingi ni mchezo tu wa kuigiza ili kuweza kuwatawala watawaliwao vyema. kiongozi aliyeko madarakani aliahiidi kuwapeleka peponi bila kulazimika kufa, lakini baada ya miaka mitano bado mnaishi kuzimu, na hapo ndipo ajapo kiongozi mwingine asiyekuwepo madarakani (mpinzani) na kukucheka kwamba ahah, huyo alikudanganya, mimi naweza kukupeleka peponi, baada ya miaka mitano wajikuta kuzimu zaidi

uongo uendelea

sasa maisha bora kwa kila mtanzania ni kama tusi kwa waliyotuahidi!

2 comments:

emu-three said...

MMMH, siasa ni uwongo wenye ukweli ndani ndani yake . jadili.
Hili ni swali la siasa nalikumbuka sana wakati nipo sekondari. Nililiona kama swali la utata kipindi hicho kwani `uwongo' na `ukweli' uweze kukaa zizi moja.
Sasa nalikumbuka sana hilo swali kwani nipo kwenye `vitendo' vyake, nawaona wanasiasa wanavyomwaga sera, ukizisikiliza utasema mmmh hizi ndizo sera!
Sasa wape madaraka, utakumbuka ule usemi wao, ambao mmmh, uliuona ukweli , sasa mmmh, umegeuka uwongo!

SIMON KITURURU said...

Mmmh!