Saturday, November 27, 2010

tamaduni zetu na ubini wetu, sasa baba katikati??

ndugu mimi nashindwa kuelewa kidogo tamaduni za kitanzania lijapo suala la ndugu wa kiume wa baba yako, kwa mfano kuna baba mdogo na baba mkukbwa harafu na baba tu au baba katikati?

sasa mimi ni mtoto wa mwisho katika uzazi wa marehemu mzee wangu, tuko wavulana watatu na wasichana watatu, ila sasa kati ya watoto wa marehemu mzee wangu mimi ndiye wa kwanza kupata mtoto, mtoto mwenyewe ni wa kiume kwa hiyo ndio mjukuu wa kwaza wa mzee kutoka katika uzazi wa kiume au wanaoendeleza ukoo!

ila sasa, ngoma nzito, mwanangu atawaita kaka zangu kuwa baba mkubwa, then sina mdogo kwa hiyo mimi ndo niwe baba mdogo au baba katikati?? yaani kwa mtizamo usiokuwa wa kiutambuzi na kwa mtizama wa kutafuta vyeo vya kidunia, mimi nazaa harafu nakuwa mzazi mdogo?

utambulisho wangu kwa mwanangu kwa ndugu yangu yeyote wa kiume utakuwa ni BABA MDOGO no matter how many years one may be ahead of me, au sio mazee??

5 comments:

emu-three said...

Ndi hivyo baba mdogo we ulitakaje? manake kwa mimi nionavyo, baba mdogo manake kuna nudgu zako mbele, ndio maana we waitwa ba-mdogo! Au? Unajua tena leo wikiendi, nasoma huku natizama bosi asije akaingia ghafla...tehetehe

Anonymous said...

Kuna baba mmoja tu...biological (mzazi).

Ndugu zake wakubwa ni baba wakubwa wakifuatiwa kila mara na majina yao.

Ndugu zake wadogo ni baba wadogo wakifuatiwa kila mara na majina yao.

Hii pia inagusa mama.

Koero Mkundi said...

Nadhani tungetumia neno mjomba kama wadhungu...sijui naeleweka?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony umenena, japo watu hufupisha hawatamki majina, ila wataitwa ba-mdogo nanii sio mkubwa

Anonymous said...

sisi wahaya hatuna baba mkubwa tuna baba mdogo regadlees katangulia kuzaliwa.ichwe twina tatento na tatakinzala upo hapo kamara?????sasa ukitaka kuiga vya wenzako uonekane umesoma utachemsha na ndio maana mtoto wa shangazi yangu ananiita mjomba busara za wazee wetu wa zamani