Monday, November 29, 2010

tuanze sasa kuhusu Mungu a.k.a Sir God

nimekuwa nikiyategea maswali yaliyowahi kuulizwa na damija siku za nyuma sasa sina jinsi ila kujiingiza ukumbini na kuanza kuyajadili. moja wapo ni kuhusu Mungu au nguvu kuu

sasa basi sula la kimungu lina mitizamo lukuki, kuna mtizamo wa kiutambuzi, wa kidini, wa kipagani, wa kisayasi, na mingineyo

labda tuanze kwa maswali tu, wewe wafahamu Mungu ninini, ni kitu gani?

je ni hisia gani zinakuhijia litamkwapo neno Mungu? ni woga, hofu, hukumu? kifo? moto wa milele au maraha tele?

lakini twaweza kushi ki-Mungu?

je amri, sheria au kanuni za Mungu ni zipi?

ni mwanzo sasa!

4 comments:

emu-three said...

Mungu wengi twasema twamjua, na wengi wasema twamfuta na wengi wasema ni `watakatifu, walokole, wachamungu..'
Lakini je ni kweli, `angalia matendo yao, yatakupa jibu!
Mungu ni jina ambalo twajua ndiye muumbaji, wengine wanamuita tofauti, lakini maana pevu ni kuwa yeye ni muumbaji, mwenye mamlaka yote na akitaka liwe yeye husema kuwa na huwa!
Lakini mmmh, kila mmoja anambwembwe zake za kumwabudu, hutaamini kuwa kuna wanaomnasibihs mungu na kitu, mtu au vitu...sijiu, hapo naona twamtilia mungu `udhaifu usio wake...' yeye akitaka kitu kiwe husema kuwa na huwa...sasa kwanini ajizalilishe, na kuwa kitu, mtu au...kwakweli mimi sijui!
Ni hayo tu mkuu!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mungu ni pendo,

Mungu ni uhai,

Mungu ni moto ulao,

Mungu ni hakimu....

Mungu ni mwokozi (Yesu ni Mungu ati!)....

Na kuna wanaodhani kwamba wanammiliki Mungu kiasi cha kuwatoza wengine pesa ili huyo Mungu awasamehe dhambi zao au kuwabariki. Hapa Marekani hii ni biashara kubwa sana. Kuna wanaouza maji ya baraka, vitambaa vya mfukoni vyenye upako, vipande vya mikate vyenye mibaraka n.k. Bei ni dola 1000 tu na hapo basi kaa usubiri mibaraka itakavyokumiminikia! Madeni yako yatafutwa, kazini utapandishwa cheo, mke/mme wako hatakuacha n.k, n.k, n.k......

Hakuna anayemjua Mungu na jibu limeshatolewa na emu-three hapo juu! Wote tunapapasa tu na kama wale vipofu watatu waliokuwa wanampapasa tembo, kila mmoja anamtambua Mungu kivyake....

Mada nzuri. Nasubiri kuona walokole watasemaje.

Mija Shija Sayi said...

Mungu halisi ni mmoja, ila photocopy ndio wengi sana. Hawa photocopy ndio huwa na visa vingi kama alivyosema Kaka Matondo na M-3hapo juu. Hivyo tunabidi tuwe makini tunapoongelea juu ya Mungu ili tujue tunamuongelea yupi Copy au Halisi ambaye kumfikia yeye ni lazima utumie password ya jina la Yesu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duhu, natuone mada inavyoendelea ila passwed????