Thursday, November 18, 2010

ubatizo mana yake nini? au kwa manufaa ya jamii!

katoto kangu kapendwa sasa kanazidi kuwa kakubwa na nakuzidi kuimarika katika ulimwengu huu wa kuigia unalia na kutoka unachekelea. sasa basi mimi naishi katika eneo la dini au misheni, ila nipo pale kimaslahi tu na si vinginevyo

ila sasa changamoto nikutanayo nayo ni ubatizo wa kijana wangu. kila mtu anashangaa eti sijambatiza mpaka sasa. sasa sijui haraka ni ya nini au nisubiri tu akiwa mkubwa yeye achague dini apendayo na kuisujudia hiyo

mimi nakutana na maswali magumu juu ya kwa nini nilichaguliwa dini nikiwa bado mduchu, hivi ni lazima kweli kumbatiza mwanangu na kumfuatisha dini fulani kwa utashi wangu? je sivyema kumwacha yeye akiwa mkubwa atachagua dini aipendayo na kuifuta hiyo? nani kalazimisha watu kufuata dini za wazazi wao?

najiuliza tu, lakini hata ubatizo wenyewe kibiblia ni utamaduni tu wa waYahudi kuliko wakovu wenyenwe. tunaona au kuambiwa ya kuwa Yesu alikuja na ubatizo ulioendelea kuliko wa Yohana, yeye alikuja na ubatizo wa ROHO na KWELI na sio ule wa maji, na katika simulizi za bible, hakuna pahala yesu anabatiza kwa maji, ila kwa kusali, na kumjua Mungu, kwa Upendo na kutokuhukumu, sasa wapi na wapi tuamini kuwa ubatizo ni sehemu ya mafundisho ya Yesu ?

najiuliza, kama kuna ushauri na ushawishi, basi mwanangu atabatizwa, ila majina yake sasa sijui kama wabatizao wataweza kuyatamka maana duhu

6 comments:

Anonymous said...

wewe kamala vipi siumeisha mpa jina huyo mtoto? ndo umeisha mbatiza kama ni swala la maji si anaogakilasiku? kwani mababuzetu wa zamani walibatizwa mbona waliishi vuri na kuheshimiana achakasumba ya kuiga vya wazungu

SIMON KITURURU said...

Mmmh!

Upepo Mwanana said...

Nahisi upagani wangu bado unafaa, hizi dini zinachanganya tu. Maadili mema ya asilia ndio maisha ninayoyataka na kuyafuata.
Natumaini sijamtukana mtu hapo

Anonymous said...

upepo mwanana hujatukana umesema vema mimi hata matambiko yajadi yaani dini zetu za asili ninafanya tena safi nawatu wanafurahia

Mzee wa Changamoto said...

Tough one.

Anonymous said...

Unajua binadamu ana mambo na vijambo vingi sana kiasi wakati mwingine vurugu tupu. Ubatizo kwangu ni utaratibu wa kimazoea kama zilivyo taratibu nyingine. Ingawa kama yalivyo mambo mengine ni swala la wewe unasemaje. Ukiona linafaa fanya au la acha. Swala la jina nalo hivyo hivyo! Wanabatiza ndio waamuzi itabidi ukubaliane nao vinginevyo hataingia mbingu!!!