Friday, December 10, 2010

dini huleta amani au chuki?

wanadai kuwa " God made mn in his own image, man made religion in his (man) own Image and religion mane God in its own image"

hivi kweli dini huleta amani duniania au chuki, ubaguzi na ubinafsi? angalia vita vikuubwa vyote vya dunia, kama vile Israel na palestine, Darful, na hata kwenye historia, unaona amani kutokana na udini??

kwenye jamii yako je, kuna amani au vurugu tupu?ubaguzi wa kidini umejaa, hata kwenye Nyumba za Ibada, kuna amani kweli? si ni ubaguzi wa ashirikiye meza ya bwana na asiyeshiriki? atoaye sadaka kubwa na ndogo? au?

sasa eti dini inaleta amani, tuangalie jamii za kiafrika kabla ya ujio ya dini, na hadaa nyingine, je ziliishije? kwa amani au vurugu? mbona hakukuwepo na yatima, ubaguzi wa ajabu nk?

ni swali, dini inaleta amani au vurugu na mauaji?

2 comments:

Mbele said...

Inaweza kuwa taabu kufafanua dini ni nini. Lakini ngoja nitumie dhana ambayo tunatumia katika mazungumzo ya kawaida, tunaposema mimi Mkristu, Muislam, Msabato, Mlokole, Mhindu, na kadhalika.

Naamini kuwa penye dini panakuwa na amani, upendo, na kuvumiliana. Haya ndio matokeo ya kuwepo kwa dini, na ndio uthibitisho wa kuwepo kwa dini.

Vita na migororo ni ushahidi kuwa hapo mahali hapana dini. Dhana ya mgogoro wa kidini au vita vya kidini ni dhana ya kitapeli au kifisadi, kama nilivyodokeza hapa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hivi prof uazishwaji wa din wenyewe sio usanii au utapeli? tuone historia za dini hizo

mimi naona kama dini nyingi kama sio zote ni hadaa tu