Thursday, December 16, 2010

Kama Mungu ni pendo, twapendaje?

Kuna madai mengi ya kuwa Mungu ni pendo. Vitabu vyoote vya dini huongelea habari hizi za Mungu ni pendo na upendo wa Mungu, vitabu hivyo vimeongelea sana juu ya sifa za upendo lakini kwa bahati mbaya havijatuwezesha kupenda hata kidogo

Tena kwa sababu ya dini hizo kuongozwa na wasomi ambao hawajawahi kukua kiroho na hivyo ujua kunukuu, upendo huo umegawanywa katika makundi kwamba umpende mwana dini yako tu au mtu Fulani

Kumpenda mtu ni nini na twampendaje?
Upendo wa kumpenda mtu ni kumchukulia na kumkubali pia kumpokea kama alivyo bila masharti wala kutaka kumbadilisha. Ukimpenda mtu utamkubali pamoja na udhaifu wowote ule alio nao. Upendo ukiwa na masharti huo sio upendo tena bali vitu vingine

Katika maisha yetu ni lazima tujifunze kukubaliana na kupokeana kama tulivyo, hapo twampenda huyo na kumpenda Mungu aliyemuumba hivyo huyo tumpendaye

Ili tuweze kuwa pamoja na Mungu ni lazima kwanza tuyapenda mazingira yanayotuzunguka, tumpende jirani, tupende hata vitu vingine bila kutaka kuvibadilisha sana, kwa mfano, kamamhali ya hewa ni joto sana, ni lazima tuikubali na kuipokea hali hiyo kama ilivyo kwani hatuwezi kuibadili, hata baridi, mvua au jua kali hivyo hivyo


Ni lazima tuzipende, yaani tuzipokee kama zilivyo badala ya kulalamika ambako hakutotusaidia chochote kwani hutabadili kitu, hiyo itakuwa hatua ya kwanza ya Kumpenda Mungu pia

UPENDO


1 comment:

emu-three said...

Mungu ni UPENDO, Mungu ni AMANI, Mungu ni HAKIMU...Kwangu mimi mkuu hizo ni sifa,au majina ya Mungu kutokana na sifa zake. Lakini sisi wanadamu tulitakiwa tuwe na sifa hizo anagalau chembe moja kama chembe ya tone la maji katika bahari! Tumeshindwa...labda mimi sio mtaalamu sana wa haya, au...Mkuu ni hayo tu!