Friday, December 17, 2010

kama yesu Kristo Angeishi leo.........

katika pitia pitia yangu nimekutana na changamoto kuubwa juu ya ukristo na maisha ya ukristo na Kristo mwenyewe. kuna watu wengi sana wanaoamini kuwa ni wafuasi wa Kristo. wengine hujiita watumishi wake na wengine wafuasi

kuna dini lukuki za Kikristo, makundi kama vile walokole, wana maombi nk

ila sasa swali kubwa la kujiuliza hapa ni kama kweli huyu kristo mwenyewe angekuwa bado anaishi leo au angerudi, unadhani huwa wajiitao wafuasi wake wengemkubali kumpokea na hata kumfuata? si wangemuona mwendawazimu falani?

unafikiri kwanini alikataliwa, kupigwa na kuuwawa kama angefuatwa? anafutwa sasa kwa sababu hayupo duniani lakini angekuwepo bado ingekuwa soo kwa wengi kwani angewasumbua sana

unafikiri angekubali makundi ya kibaguzi eti ni dini? je mfumo wa kanisa? si tunaona anatimuliwa kanisani / hekaluni kisa anavuruga utaratibu wa vibosile fulani? si anawatukana walimu na wakuu wa dini? si tunamwona mtaani akiongea na machangudoa, walevi na wapiga debe?

unadhani angekuwa kama papa mwenye kusoma hotuba au angekuwa mwenye uwezo wa kuongea bila rejea?

hii ni sawa na nyerere, watanzania wengi hujiaminisha kuwa ni wafuasi wa nyerere, lakini kama nyerere angalikuwa madarakani leo hao wangekuwa walalamikaji vibaya na kumuepuka

kwa kifupi tunapenda mazuri ya watu wema au waliouishi wema lakini hatuko tayari hata kidogo kuwa wema!

yesu rudi uone watu wanavyokusingizia!

AMEN

4 comments:

SIMON KITURURU said...

Kuna starehe ya kufuata WAFU kwa kuwa nasikia kuna waliofuata waliohai na kustukia wametongozwa!:-(

Wafu unaweza kuwatungia stori au KUISHEPU TARALILA YAO ieleweke vingine na WASIKUBISHIE .:-(

WAFU oyeee!

Yasinta Ngonyani said...

Simon:-)

Hakika ni kweli tenda wema nenda zako usingoje shukrani duniani hapa. Kamala nimependa hii kuwa kwanini watu wampemtu wasifu wake wakati angali hai?

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Ni unafiki wetu binadamu kusubiri watu wafe ndiyo tuanze kuwamwagia sifa kemkem hata kama tulikuwa hatuwapendi walipokuwa hai.

Hitimisho lako nakubaliana nalo. Ndiyo maana huwa nashangaa ninapokutana na mtu anayejinadi eti mlokole na anadai ameokoka lakini amekosana na ndugu zake mpaka kufikia hatua ya kutosalimiana nao. Na wakati huo huo Yesu Mwenyewe anayemfuata alitufundisha kusameheana na kupendana kwanza sisi kwa sisi kabla hatujaomba kusamehewa dhambi zako.

Kama Yesu Angeishi leo angeona mambo sawa na yale yale aliyoyaona wakati ule alipoishi kwani kimsingi hatujabadilika. Wengi wetu bado tuko binadamu wale wale aliowaacha - hata kama tunajidai kwamba tunamfuata na kujipachika vyeo mbalimbali kama ulokole, unabii, utume, utakatifu n.k.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

typo...

kabla hatujaomba kusamehewa dhambi zako isomeke kama

kabla hatujaomba kusamehewa dhambi zetu.