Wednesday, December 1, 2010

majina ya kile/yule aitwaye Mungu

sijui nini hasa chanzo au maana ya neno Mungu hata lile la kiingereza God na kwahiyo sielewi maneno hayo yana uzito gani yatamkwapo kumaanisha kile tutakacho kuelewa

ila sasa neno tukiangalia maana au majina mengineyo ya yule tumwitaye Mungu twapata majibu tofauti au maana kubwa zaidi na za kueleweka

wapo wapendao kumwita Mungu kuwa ni uwepo mkuu (supreme being), au kwa mtizamo wa kisayansi unaoamini nguvu basi huita Nguvu kuu (omnipotent, omnisicient, omnipresent) nk

mimi napendelea kutumia uwepo mkuu au nguvu kuu kwani ukiangalia kwa uhalisia ni kwamba sisi (binaamu) na viumbe vingine ni nguvu na ni uwepo, lakini kuna linguvu likubwa zaidi yetu, tuliite nguvu kuu, kama sisi ni uwepo mkuu, basi pia kuna uwepo mkubwa zaidi yetu na hivyo twaweza kuita uwepo mkuu

katika mjadala huu, tutatumia jina Mungu kwa kuwa ndilo lililo zoeleka kwa wengi kumaanisha yote hayo

itaendelea

2 comments:

emu-three said...

Ngoja nitafakari kidogo:
Mungu alikuwepo na atakuwepo, ni nani alisema tumuite Mungu? Mimi kwa jibu la mkato ni `VITABU VITAKATIFU'
Lakini mababu zetu kabla ya kuingia dini humu nchini walikuwa wakimjua mungu, lakini labda sio kwa jina hilo tunalolijua sasa...wao walipta wapi wazo hilo, na jina hilo?
Kwa mtizamo wetu rahisi ni kuwa maswala haya yamejengwa ki-imani. Na imani ndiyo inayomjenga huyu mtu `aogope' kutenda ovu, aogope kuwa hata nikiwa peke yangu siwezi kufanya hili kwasababu ya imani kuwa ipo nguvu inaniona!
Fikiria leo kama imani ya mungu isingekuwepo dunia ingekuwa wapi?
Oh, ni hayo tu mkuu

SIMON KITURURU said...

Majina kwa kawaida ni udhaifu wa BINADAMU tu!

Binadamu angekuwa si dhaifu LABDA asingehitaji kuwa na MAJINA kama viumbe vingine visivyohitaji kuwa na majina.


SI unajua karibu wanyama wote duniani hawaitani kwa jina ila hutambuana kuwa nani ni nani?

Ukifikiria toto la njiwa lijuavyo mama ni nani kama toto la PENGUINE, hujawahi kusisi la bda kuwa na jina ni udhaifu?


Unafikiri kweli jina la MUNGU ni lipi ukizingatia labda kila lugha duniani inamuita jina jingine kuanzia GOD, Mugnu, Mrungu, Umkama,JAH, YEHOVA, Alla......

hasa ukizingatia wewe ungeitikia jina gani kama kila mtu angekuita jina jingine?


Nawaza tu kwa sauti!:-(