Thursday, December 2, 2010

majina ya Nguvu / uwepo mkubwa au Mungu

ilishasemwa hapa kijiweni juu ya baadhi ya majina ya yule aitwaye Mungu sasa kuna majina mbali mbali kufuatana na tamaduni mila na desturi. kwa kifupi sijui nini hasa maana ya neno la kiswahili Mungu au la kiingereza God, kama kuna ajuaye na atueleze basi

ila kuna majina ya kihaya ya Mungu na maana yake kama vile:

Katonda == muumbaji

Lugaba == mtpaji / mpaji

Lubaho == anayejali

Nyamuhanga / Luhanga == anaye sema na ikawa

hayo ni baadhi yamajina ya kihaya ya maanishayo Mungu kuna hata mengine ya kiswahili kama vile Muumbaji, mwokozi, nk

je kikwenu au kivingine kuna majina ya Mungu na maana yake? ni yapi? siri kubwa katika majina haya tunaona ikiwa zaidi ni ukubwa, wa kila kitu ni

next ni Mtizamo wa Mungu kwa dini zetu

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kamala mbona majina mengu hivyo na yote hayoo yanamaanisha Mungu? mmmhh kikwetu Mungu ni Mungu tu...lol

emu-three said...

Kikwetu mungu anaitwa `mrungu' wengine wanaita `mfumwa'...mmmh, maana hasa ni utukuzo!

chib said...

Mungu ni Mungu tu. Hata ukiita jina gani. Sifa za huyo Mungu zipo sawa.
Ni sawa na Maji. useme amazi(apology here kwa kihaya fulani ina maana nyingine), water, waser, amanji, amashugi, mayi, obinyo nk, yote ni kitu kimoja tuuuu
Nimeogopa kutolea mfano wa neno Mungu kwa Kinyarwanda, maana Kamala atafumuka huyooooo, atasema nimewadharau wanawake wote, am serious here

SIMON KITURURU said...

M3 kanisemea kikwetu kwa lugha ya BABA. Kijita lugha ya MAMA nimesahau Mungu anaitwaje mpaka nimkong'olee simu MAMA na kwa bahati mbaya napokusoma ni saa tisa usiku sasa hivi ambavyo sina wakumkongolea nimjuaye MJITA mwenye mchezo wakuwa macho usiku hivi.:-(

Wajita Mpo mniingizie JINA la Mfumwa?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@chib, amazi??? tuheshiiane, sio maji ni uchafu huo na amashugi?? ni yale yanayo slide

chib said...

Ndugu yangu Kamala, kinyarwanda nilichojifunzia huku, amazi ni maji tena safi kabisa, ndio maana nilitanguliza appology kwa akina nshomile, na ndio maana nilikataa pia kutaja neno Mungu kwa kinyarwanda, maana nilijua utang'aka mara kumi zaidi ya hii he he heeee

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

@Chib hata kwa kida ni hivyo kikwetu ni vile vyakula ulivyokula jana!!! Mungu kwa kinyarwnda si ni Imana?? wakati kikwetu ni ile ishu ikuhangaishayo kujua kama inatolewa nje / mbali yako??

Mzee wa Changamoto said...

Duh!!!!!!!
Kweli kuna haja ya kujifunza ki-"kwao" kabla ya kuongea. Myarwanda akija kwetu akasema Mungu ni kama maji (kikwao), watu watamkimbia wakimlaani
Hahahahaaaaa