Friday, December 3, 2010

Mungu kwa mtizamo wa dini zetu

tuangalia juu ya yule au kile kiitwacho Mungu kwa mtizamo wa dini zetu, nisemapo dini zetu kwa kifupi naongelea uislamu na ukristo lakini na labda kuna dini za asili

kuna biblia na koran ziongeleazo Mungu na huitwa vitabu vitakatifu au vitukufu vya Mungu au "neno" la Mungu, hapa swali huzuka, hivi Mungu ana tujimaneno tuchache twa kuishia kwenye vitabu vidogo namna hile?

kuna vitabu vingine viongeleavyo habari za Mungu, baadhi ya vitabu vya dini za Asia huwa navifagilia kiasi fulani. tunaona vitabu kama vila bhagavadi gita, granth sahib, adhi grandh, nk, vitabu va asia huongelea Mungu kwa mtizamo unaoeleweka kuliko vitabu vingi tuvijuavyo

kwa mtizamo wa Bible Mungu ni baba, ni mmiliki wa kila kitu, ni Muumbaji, ni HAKIMU, ana moto wa milele, ana wivu, ana hasira, ana mtoto mmoja tu wa kiume, kuna watu ambao hawapendi na hvyo huwauwa kupitia vita. ana taifa moja teule tu la Israel lenye nguvu ya kivita nk habari zake hujulikana kupitia wasomi kama wachiugaji, maaskofu nk, kuwahoji hawa ni kufuru mbaya sana

kwa mtizamo wa Korani huyu ni ALLAH, hana uhusiano wa kibaiolojia na yeyote ila atahukumu na anakihama, habari zake ujulikana kupitia kwa wasomi wake kama masheikh, ma-Imam nk, ana mavazi rasmi matukufu, huongoza Jihad dhidi ya wasioendana na matakwa yake nk

kwenye vitadu vinginevyo, Mungu hufkiwa kwa tahajud / meditation nk! napenda vitabu hivi

tutaendelea

1 comment:

chib said...

Leo, no comment!