Tuesday, December 14, 2010

Mungu na utupu, nothingness au nuru

Katika kudodosa juu ya mungu tunajikuta na utupu au nothingness. Mungu si kitu wala mtu bali ni utupu au nothingness ambao upo katika kila kitu (manifested in everything)

katika hewa tunakuta Mungu ambayo yatufanya tuwepo, katika ardhi twakuta mtoa uhai pia na katika maji na kila kitu

ndani mwetu kama binadamu na viumbe vingine kuna utupu pia ambao ndio uhai wenyewe au sisi wenyewe na kila pahala

Mungu ni-formless lakini pia akilazimika kuelezeka katika vitu basi hulazimika kuwa katika mfumo wa mwangu (nuru) na hata sauti (sound)

ndio maana katika vitabu vya dini twaitwa nuru ya ulimwengu lakini pia kuna sauti kadhaa za Mungu nk kama vile radi, upepo nk

ndio maana t unaona waanzilishi wa dini wakijitenga na kubakia pekee yao ili wapate utupu na kurudi kwetu na uwezo na habari kibao njema

tunamwona Kristo akiwa milimani au bustanini peke yake ili kupata maagizo na uweza zaidi nk

ndani mwetu hatuchoki kuingiza na kutoa utupu kwa njia ya kupumua na hivyo kuendelea kuishi

2 comments:

emu-three said...

Kwangu mimi kwa mtiamo wangu finyu nahisi Mungu yupo, na sio `utupu' kwani ukiwa peke yako, yeye yupo, nawe. Yeye yupo kila mahali,ila huwezi kumuelezea, kwani yeye hana umbile.
Atakuwaje na umbile wakati yeye ndiye kakuumba. Hawezi jujizalilisha kwa kitu kidogo alichokiumba yeye, ndio maana narudi tena ule usemi usemao,
Utafananisha na nini ili awe sawa naa yeye...hakuna! Yupo lakini kwa akili zetu hatuna uwezo wa kumuelezea alivyo!
Hivyo ndivyo

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duhu kama hana umbile ninini sasa? kumbuka kuna vitu anavyojeielezea